Ushirikishaji wa Wadau

Kwa mashirika ya eneo yanayopanga mradi wa P/CVE, usaidizi na kushiriki kwa wadau muhimu wa eneo (ikijumuisha wanajamii na viongozi) ni muhimu zaidi.  Pia, mashirika ya eneo yanaweza kuendeleza zaidi malengo yake ya mradi wa P/CVE kwa kukuza uwezo na kujitolea kwa wawakilishi wa eneo na serikali katika kukabiliana na shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu na kwa kuwajibisha serikali. Mradi wako unaweza kushirikisha wawakilishi wa eneo kwa “kubuni pamoja” shughuli za mradi, kutekeleza mabaraza ya kukusanya maoni na mafunzo na kuhimiza uwekezaji (vitu halisi au visivyo halisi) wa wawakilishi wa eneo katika shughuli za mradi.

Unaposhirikisha wadau wakati wa awamu ya utekelezaji wa mradi, rejelea Sehemu ya Jumla kuhusu Ushirikishaji wa Wadau.

Title
Mpango wa ushirikishaji wa wadau wengi unafananaje?

Stakeholder engagement plans must be tailored for each project. For P/CVE projects, local dynamics and context play a critical role in shaping the project design, and therefore the local system actors who should be engaged. The following guiding questions and sample outlines will help you develop an effective stakeholder engagement plan.  

NANI? Ni wadau gani ambao wanapaswa kupewa kipaumbele na kushirikishwa kulingana na shughuli za kwanza za ukadiriaji na ubainishaji wa wadau? Je, makundi yoyote yaliyotengwa yametambuliwa kati ya wadau hawa? 
KWA NINI? Malengo na maslahi ya kila mshika dau ni yepi? Ni nini ambacho kimewatia motisha wadau kushirikiana nawe? Kwa nini wadau wanashirikishwa?
NINI? Kina na upana wa kushiriki kwa kila mshika dau katika kila hatua ya mradi ni kipi? Maamuzi ya kimkakati ambayo yanahitaji kufanywa kwa pamoja ni yepi?
VIPI? Mbinu za kushirikisha kila mshika dau ni zipi? Ni mkakati gani wa kuhakikisha kwamba makundi yaliyotendwa yameshirikishwa?
LINI? Wadau watashirikishwa mara ngapi na kwa muda gani?
MAJUKUMU? Wawakilishi wa wadau watatekeleza jukumu gani? Ni nani atakayesimamia mchakato wa ushirikishaji wa wadau?
NYENZO? Mpango wa ushirikishaji wa wadau utagharimu nini na kulingana na bajeti ipi?

 

KIDOKEZO CHA UTEKELEZAJI

MFANO WA MPANGO RAHISI WA USHIRIKISHAJI WA WADAU

Kwa kutumia mfano huu, unaweza kuorodhesha wadau wanaoweza kushirikishwa, kutambua nia yao ya kutaka kushiriki, jinsi mchakato wa ushirikishaji utakavyoendelea, atakayeusimamia, wakati gani na jinsi utakavyofadhiliwa/kufanikishwa.

Mshika dau (mtu au kikundi) Nia/Malengo ya Mshika Dau Njia za Kushiriki Wajibu wa Kushiriki Muda Kadirio la Gharama (jumuisha nyenzo)
           
           
           
           
           
           

 

MFANO WA MPANGO WA KINA WA USHIRIKISHAJI WA WADAU

Ikiwa una muda wa ziada, zingatia kubuni mpango wa kina wa ushirikishaji, kama ilivyofafanuliwa hapa chini:

1

MAELEZO YA MRADI

Sehemu hii inapaswa kutoa kwa ufupi muhtasari wa mradi (malengo, ukubwa wa eneo, Nadharia ya Mabadiliko, n.k.) ikijumuisha changamoto za kimuktadha zinazoweza kutokea.

2

WADAU WA MRADI

Kulingana na utambuzi/uchanganuzi wa wadau, tambua makundi ya wadau muhimu watakaoshirikishwa katika mradi. Jumuisha watu au makundi ambayo:

  • Yanaathiriwa moja kwa moja na/au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na mradi na/au shughuli zake
  • Yamebainisha “nia” zao za kushiriki katika mradi
  • Wanaweza kuchangia katika matokeo mradi au ufanisi wa utendakazi

Fafanua ni kwa nini umeamua kushirikiana na wadau hawa. Ni nini kusudi la kushirikiana na kila mtu au kikundi?

3

MPANGO WA USHIRIKISHAJI WA WADAU

  • Toa muhtasari wa kusudi na malengo ya mpango wa ushirikishaji wa wadau. Kwa nini unahitaji mpango huu na utautumiaje?
  • Fafanua kwa nini wadau mahususi (watu binafsi au makundi) wamechaguliwa ili kushiriki katika mradi. Ni nini kusudi la ushirikiano huu?
  • Fafanua kwa ufupi maelezo yatakayoshirikiwa na wadau, katika muundo na lugha gani na njia gani zitakazotumiwa kushiriki maelezo.
  • Orodhesha vitendo/shughuli zozote za ushirikishaji ambazo zitatokana na ushirikiano rasmi, mafunzo na shughuli za ukuza wa uwezo, kampeni za uhamasishaji n.k.
  • Fafanua njia zitakazotumiwa kushirikisha kila kikundi cha wadau kilichobainishwa.
  • Fafanua hatua mahususi zitakazochukuliwa ili kushirikisha makundi mbalimbali (ikijumuisha wanawake, dini au kabila za walio wachache, vijana na makundi mengine yaliyotengwa).
4

RATIBA

  • Weka muda/ratiba ambayo inabainisha tarehe/mara na maeneo ambapo shughuli mbalimbali za ushirikishaji wa wadau zitafanyika, ikijumuisha mashauriano na ushirikiano.
5

NYENZO NA WAJIBU

  • Bainisha wajibu wa kila mshika dau katika utekelezaji wa shughuli za mradi.
  • Bainisha bajeti na nyenzo nyingine ambazo zitatumika katika kutekeleza shughuli hizi.
  • Bainisha atayeratibu na kusimamia mpango wa ushirikishaji wa wadau.
6

UFUATILIAJI NA KURIPOTI

  • Bainisha jinsi wadau watakavyohusishwa katika ufuatiliaji wa shughuli za utekelezaji wa mradi.
  • Bainisha jinsi na wakati ambapo matokeo ya shughuli za ushirikishaji wa wadau yatashirikiwa na makundi makubwa ya wadau (k.m., majarida, ripoti za ukadiriaji, ripoti za ufuatiliaji na utathmini, mikutano na matukio, n.k.).
  • Bainisha mchakato utakaotumiwa na watekelezaji kukusanya maoni ya wadau (ikijumuisha wale ambao wanaathiriwa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na mradi). Bainisha jinsi changamoto zitakavyoshughulikiwa.
Title
doc
ZOEZI LA MPANGO WA UHUSIANO NA UCHAGUZI
photo
Details

Karatasi ya Kazi ya Mpango wa Ufikiaji na Uchaguzi

Mara tu unapochagua washikadau wa kushiriki, laha-kazi hii inaweza kukusaidia kubainisha hatua muhimu za shirika lako kufikia na kutambua vikundi lengwa vya shughuli zako.