Viashirio

Vifungu viwili vinavyofuata vitaangazia viashirio na njia za uthibitishaji. Viashirio thabiti vitatoa vipimo vya ubora na takwimu za kina kuhusu athari na mchakato wa mradi. Njia za uthibitishaji inamaanisha jinsi utakavyopata data inayolingana na kiashirio husika.

logframe

Viashirio ni nini ?

Viashirio ni vipimo vya ubora au takwimu za kina za aina na mchakato wa mabadiliko. Katika miradi ya PVE ambapo mabadiliko ni changamano na yanahusisha mitazamo, tabia na mahusiano, ni muhimu kuweka mpango na kufuatilia mabadiliko ya ubora. 

Kwa nini unapaswa kuvitumia ?

Viashirio ni muhimu katika kutufahamisha aina ya data inayopaswa kukusanywa na vitatupatia maelezo kuhusu wakati, jinsi na njia ambazo zinapaswa kutumika katika ukusanyaji wa data hiyo. Hata hivyo, ni baada tu ya data kuchanganuliwa ndipo tutakapoelewa mabadiliko yaliyotendeka. Uchanganuzi bora inamaanisha uthibitishaji wa data, yaani kuthibitisha data kutoka kwenye angalau vyanzo vingine viwili na kutumia mseto wa mbinu, kama vile kujaribu mtindo wa takwimu za data kwa kutumia data iliyokusanywa kupitia mazungumzo ya kikundi lengwa na maoni ya mtoa habari muhimu. 

*Ufafanuzi wa hapo juu umetolewa katika shirika la UNDP/International Alert

 

Viashirio vya takwimu za data dhidi ya viashirio vya ubora wa data

 

indicators

 

Nyenzo hii kutoka katika shirika la United States Institute of Peace inabainisha sehemu chache muhimu ambazo miradi ya P/CVE inapaswa kukadiria mabadiliko yaliyotendeka katika: mitazamo, tabia na mahusiano.

Mitazamo

Inaweza kukadiria:

  • Mabadiliko katika dhana za kijamii, kisiasa na kiimani zilizoshikiliwa na watu wanaolengwa na mradi, ikijumuisha mitazamo yao kuhusu matumizi ya vurugu na misimamo yao ya kidhana.

Kwa kawaida hukadiriwa kupitia:

  • Kukadiria maarifa ya mtu kuhusu suala la shughuli za VE, pamoja na jinsi anavyolichukulia.

Mapungufu:

  • Kipimo hiki kinatokana na dhana ya msingi kuhusu uhusiano kati ya dhana za makundi yenye itikadi kali na shughuli ya vurugu Si wote wanaoshikilia dhana za itikadi kali ambao hujihusisha katika, au hata kuunga mkono shughuli za vurugu.
Tabia na shughuli

Inaweza kukadiria:

  • Mabadiliko katika hali ya mtu kujihusisha na makundi na shughuli za VE (ikijumuisha kukubali propaganda za makundi ya shughuli za VE na kushiriki mtandaoni).
  • Mabadiliko katika hali ya kushiriki kwenye vitendo vya amani au kushiriki katika shughuli zilizobuniwa ili kukuza hali ya kustahimili au amani au kukabiliana na shughuli za makundi yenye itikadi kali. 

Kwa kawaida hukadiriwa na:

  • Tafiti mbalimbali, mahojiano, uchunguzi kifani na ushahidi usio rasmi, pamoja na kukusanya data kuhusu matukio ya vurugu.
Mahusiano na mitandao ya kijamii

Inaweza kukadiria:

  • Mahusiano na ushirikiano wa kibinafsi na watu wa nje na ndani ya jamii ya mtu binafsi au na VEO.
  • Viwango vya mshikamano, ujumuishaji na ushirikisha wa watu katika kiwango cha jamii.

Kwa kawaida hukadiriwa kupitia:

  • Mahusiano ya kibinafsi na ushirikiano wa kijamii, mara nyingi kupitia miradi ya mtandaoni ya P/CVE au kwa kutumia akaunti za mitandao ya kijamii na wanaofuatilia ili kufuatilia mawasiliano na miktadha ya kikundi.

Mapungufu:

  • Tatizo la kimaadili linaweza kujitokeza wakati wa kufuatilia mawasiliano ya kijamii ya mtu binafsi kupitia mbinu vamizi za utafiti.

Nyenzo hii kutoka Taasisi ya Amani ya Marekani inabainisha maeneo machache muhimu ambayo miradi ya P/CVE inapaswa kupima mabadiliko ndani yake: mitazamo, tabia, na mahusiano.

Title
Aina za viashirio

Kuna aina mbili kuu za viashirio: viashirio vya ufuatiliaji wa muktadha ambavyo husaidia kukadiria mabadiliko muhimu katika mazingira ya mradi (ikijumuisha vitu ambayo huwezi kuvidhibiti); na viashirio vya ufuatiliaji wa utendaji ambavyo husaidia kukadiria hatua zinazopigwa katika kutimiza bidhaa au huduma na/au matokeo ya mradi. Ifuatayo ni mifano ya viashirio vya aina zote mbili:

Viashirio vya ufuatiliaji wa muktadha

Hufuatilia mabadiliko muhimu katika muktadha ambao mradi unatekelezwa. Mabadiliko haya yanaweza kuhusiana na miktadha ya shughuli za mradi wa PVE ambayo inaweza kuathiri utendaji wa mradi au kutoa fursa mpya.

Mfano:

  • Idadi ya matukio ya vurugu kati ya jamii ya A na jamii ya B
Viashirio vya ufuatiliaji wa muktadha  

Hukadiria utendaji wa mradi dhidi ya makusudi na malengo yaliyobainishwa katika kiwango cha bidhaa au huduma, matokeo na hatimaye katika kiwango cha athari.

Mifano:

  • Idadi ya shughuli ulizobuni mwenyewe zenye malengo yanayohusiana na shughuli za mradi wa CVE katika jamii zilizo katika hatari ya kuathiriwa, mitaa, shule n.k.
  • Asilimia ya kikundi lengwa ambayo inaamini kuwa makundi ya shughuli za VE yana jukumu muhimu la kutekeleza katika utoaji wa bidhaa na huduma za kiuchumi zinazohitajika au bidhaa na huduma nyingine za kijamii katika jamii.

*Mifano mingi ya viashirio iliyotolewa hapo juu imetolewa katika CT Bureau. Kwa mifano ya ziada ya viashirio, angalia nyenzo hii ya Indicator Bank ya shirika la International Alert/UNDP, na Mfano wa Viashiria vya CVE kutoka CT Bureau.

Title
doc
Jedwali la Kazi ya Viashiria