Kuhusu

Title
Chanzo cha Mwongozo

Wazo la kubuni Mwongozo wa Marejeleo wa Mpango wa CVE wa Mashirika ya Eneo wa mtandaoni lilitolewa moja kwa moja na mashirika ya asasi za kiraia yanayotekeleza miradi ya kuzuia na kukabiliana na shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu (P/CVE). Mengi ya mashirika haya ya eneo yanayopatikana katika nchi zilizoathiriwa na mgogoro wenye vurugu hukabiliwa na changamoto za kufikia nyenzo halisi, mahususi na zinazofaa na zana zilizobuniwa hasa kwa ajili ya matumizi yake na zinazopatikana kwa lugha zao za msingi. Isitoshe, nyenzo nyingi zilizopo zilibuniwa kwa ajili ya wabunifu wa sera, wafadhili au mashirika ya kimataifa kama vile Mashirika Yasiyo ya Serikali (NGO). Nyenzo chache zinatoa vidokezo na mwongozo halisi kwa watekelezaji wa miradi ya eneo ili waige na kutumia katika jamii zao—maeneo ya mashinani zaidi. Pia, kwa sababu ya kuendelea kuzingatiwa zaidi kwa suala la kukabiliana na shughuli za makundi yenye dhana za itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu ulimwenguni, utafiti, zana na maelezo zaidi kuhusu mipango ya P/CVE yanaibuka karibu kila siku. Maelezo haya mengi yanafanya iwe vigumu kwa mashirika ya eneo kupata, kuelewa na kutumia nyenzo kwa wakati unaofaa.

Kwa hivyo, Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (US Agency for International Development (USAID) lilishirikiana na shirika la FHI 360 kubuni zana hii ili kuwapa watumiaji uwezo wa kufikia nyenzo zinazoweza kufikiwa kwa urahisi kulingana na mahitaji yao na vikwazo vya wakati kwa kutoa maudhui ya muundo wa moduli yanayoshughulikia hatua mbalimbali za mradi (Kukadiria, Kubuni, Kutekeleza, Kufuatilia na Kutathmini, Mafunzo). Mwongozo wa marejeleo unaangazia mifumo halisi ya kutumiwa na mashirika ya eneo ili kuendeleza mipango yake ya P/CVE na unatoa viungo vya kuelekeza kwenye zana au miongozo ya ziada inayopendekezwa katika kila hatua. Ili kupunguza kurudiarudia na kuiga kazi bora zaidi ambayo tayari imefanywa na watekelezaji wa mipango ya P/CVE, tuliamua kuangazia nyenzo ambazo tayari zinapatikana na kubuni maudhui mapya tu tulipogundua kwamba kuna pengo kwenye maelezo yanayopatikana hadharani.

Title
Kazi Ambayo Haitekelezwi na Zana Hii

Huu si mwongozo kamili wa mpango wa P/CVE. Ni mfano uliochaguliwa wa zana na nyenzo za mpango wa P/CVE ambazo zinaweza kutumiwa na mashirika ya eneo. Huenda kuna mifumo, mbinu na zana au vidokezo unavyoona kuwa ni muhimu ambavyo havitajwa. Vile vile, tunatambua kwamba mashirika ya eneo yana maarifa na yanaelewa muktadha wake na suluhisho. Tunataka kuhakikisha kwamba mwongozo huu unafaa na unatimiza mahitaji ya watu na mashirika mbalimbali, kwa hivyo tafadhali wasiliana nasi ili utueleze kinachokufaa zaidi. Tutasasisha mwongozo huu ipasavyo.