Vipengele vya Mafunzo na Marekebisho

Ingawa miundo na zana za kutumia ujifunzaji na urekebishaji hutofautiana, baadhi ya vipengele vya kawaida vinaweza kusaidia kujumuisha katika mbinu yako.

KIPENGELE CHA 1 – MBINU ZA MPANGO ZINAZOWEZA KUBADILIKA

Ili kuwezesha uwezo wa kurekebika, miradi inapaswa kufafanua matokeo na malengo ya kiwango cha juu, ikifuatiwa na udhibiti na mbinu za Ufuatiliaji na Utathmini (M&E) ambazo zinazingatia zaidi uwajibikaji. Hatua zinazopigwa zinapaswa kuangazia matokeo na malengo ya kiwango cha juu na kuhusu mafunzo, badala ya kuangazia mafanikio na mipango ya utekelezaji iliyobainishwa mapema. Unapaswa kujiuliza swali hili, “je, tumefanya kitu sahihi?” badala ya, “je, tumefanya kile ambacho tulisema kwamba tutafanya?”

KIDOKEZO CHA UTEKELEZAJI

Kuunganisha, kuweka tabaka, na mpangilio

Ujifunzaji wa hatua wa USAID/OTI na mbinu ya nyongeza na matumizi yao ya kuunganisha, kuweka tabaka, na mpangilio wa shughuli ni mfano wa muundo unaonyumbulika ambao unafaa kwa kujifunza na kubadilika na kufaa kwa P/CVE. Kwa habari zaidi rejelea Moduli ya Utekelezaji.

KUBUNI NADHARIA YA MABADILIKO INAYOZINGATIA UCHANGAMANO (TOC)

Katika hali ambapo kuna uchangamano wa kiwango cha juu, unapaswa kubuni TOC inayozingatia uchangamano. Mikakati inayozingatia uchangamano ni muhimu kwa ToC kwa jumla, lakini huwa muhimu hasa katika miktadha changamano. Hii inajumuisha:

  1. Kuanzisha jambo ukiwa tayari "unafahamu mwisho wake."  ToC zinazozingatia uchangamano huangazia hasa kuhusu kufafanua tatizo na kuelezea matokeo ya kiwango cha juu ambayo mradi unatarajia kutimiza, huku zikiacha kufafanua matokeo ya kiwango cha chini au ya mfano ili kuruhusu kubuniwa kwa nadharia inayosisitiza jinsi mradi unavyotarajiwa kutimiza matokeo haya.
  2. Kukiri hali zisizobatabirika.  ToC zinazozingatia uchangamano hukiri wakati kuna hali zisizobashiriwa, labda kwa sababu muktadha unabadilika kwa haraka au kwa sababu uchanganuzi zaidi unahitaji kufanywa au kwa sababu kuna vipengele vingine mno vinavyoathiri matokeo ambavyo uhusiano wake wa chanzo na athari haubashiriki au kujirudia (au vinakisiwa tu kwa kurejelea matukio yaliyopita).
  3. Kubainisha dhana zilizotolewa wakati wa kubuni mpango.  Ni muhimu kubainisha kwa uwazi dhana kuu ambazo zimetumiwa kubuni TOC.
  4. Kubuni mfumo thabiti wa ufuatiliaji.  Baada ya timu kuthibitisha sehemu ambazo hazibashiriki na kutambua dhana kuu, timu inapaswa kubuni mfumo thabiti wa ufuatiliaji ambao inaweza kuutumia ili kukadiria TOC na dhana zake za msingi wakati wa utekelezaji.
  5. Kuweka mpango wa kufanya marekebisho.  Hatimaye, timu inapaswa kuweka mpango wa kufanya marekebisho, na hiyo inamaanisha kukuza uwezo wa kujifunza na kufanya marekebisho kuanzia mwanzoni mwa mradi. 

Kwa habari zaidi juu ya kubuni mradi wako na kutengeneza TOC, rejelea Moduli ya Kubuni

Chanzo

KIPENGELE CHA 2 – KUFANYA MAJARIBIO NA KUJIFUNZA

Kufanya majaribio na kujifunza ni kipengele muhimu hasa unapotumia mbinu au shughuli nyingi ili kutimiza lengo la mradi wako, lakini huna ushahidi wa kuthibitisha shughuli moja dhidi ya nyingine (angalia sehemu ya Mafunzo Sambamba). Kuwekeza nyenzo chache (k.m., muda, fedha na wafanyakazi) ili kujaribu mbinu na shughuli mbalimbali hukuwezesha ubainishe na kuendeleza mbinu fanisi na kupata mafunzo na ikiwezekana kupunguza au kukomesha shughuli ambazo si fanisi. Kwa maelezo zaidi kuhusu mchakato wa majaribio na kujifunza unaoitwa "ujaribio usio na nguvu," rejelea blogu hii ambayo pia inaeleza jinsi upimaji mdogo unavyotumika nchini Liberia. Kama ilivyofafanuliwa katika nyenzo hii kutoka kwa Mercy Corps, majaribio, majaribio na kurekebisha mawazo mengi ni sehemu kuu ya usimamizi unaobadilika.

KIPENGELE CHA 3 – TENGA MUDA WA KUTAFAKARI NA KUJIFUNZA

Kutenga muda wa kutafakari kuhusu mafunzo yaliyopatikana na jinsi ya kuyachukulia hatua ni sehemu muhimu ya udhibiti unaobadilika. Njia za kutumia zinaweza kuwa vipindi vya “Kutulia na Kutafakari” wakati wa mikutano ya kawaida ya kukuza ushirikiano wa timu hadi warsha ya siku moja ya ukaguzi wa mradi kila baada ya miezi mitatu. Vipindi hivi vya kutafakari na kufanya ukaguzi husaidia kutambua mbinu zinazofanya kazi na zinazohitaji kurekebishwa; kuzingatia athari za mabadiliko katika muktadha au mazingira ya utendakazi; na kukadiria ufaafu wa nadharia ya mabadiliko ya mradi. Kutokana na shughuli za kutafakari na kujifunza, timu hubainisha marekebisho yanayohitajika kwenye shughuli za mradi.

KIPENGELE CHA 4 – UFUATILIAJI NA UCHANGANUZI WA MUKTADHA

Kuelewa muktadha wa eneo ni sehemu muhimu ya Awamu ya Kukadiria ya mradi, lakini pia ni muhimu kukumbuka kwamba bila shaka muktadha huu utabadilika wakati wa utekelezaji. Ufuatiliaji wa Muktadha (imefafanuliwa kwenye sehemu ya Mbinu na Zana) huwezesha timu ya mradi wako kuelewa, kushughulikia na kufanya marekebisho kulingana na mabadiliko. Ukadiriaji wa hatari na usalama na michakato ya udhibiti iliyofafanuliwa kwenya Moduli ya Kutekeleza ni hatua za kwanza muhimu za kutambua baadhi ya vipengele muhimu zaidi vya ufuatiliaji wa muktadha. Hata hivyo, shughuli za ufuatiliaji wa muktadha na uchanganuzi hazipaswi kutumika katika Awamu ya Kukadiria au ukadiriaji wa hatari tu, lakini zinapaswa kutumika katika mradi wote.

KIPENGELE CHA 5 – MIANYA YA MAONI

Maoni inahusu kukusanya maelezo na maarifa kutoka kwa wafanyakazi, washirika wa eneo, wanajamii na washiriki wa mpango. hati ya nyenzo  inapendekeza kwamba kusikiliza na kuomba uchanganuzi na maoni kutoka katika jamii ni muhimu zaidi katika kuendeleza juhudi za kukuza amani katika eneo, mbinu ambayo pia inatumika katika nyanja ya miradi ya P/CVE. Mwanya fanisi wa maoni huanza na ukusanyaji wa maoni na uchanganuzi na inahitaji “kufungwa kwa mwanya” kwa kutambua kisha kuchukua hatua ya kurekebisha. Mianya ya maoni inaweza pia kuwa na jukumu muhimu katika Ushirikishaji wa Wadau. Nyenzo hii inaonyesha kwamba wakati washikadau wanaelewa na kuchunguza jinsi maoni yao yanavyofahamisha muundo wa mradi, ununuzi wa nguvu zaidi hutokea, ambayo hatimaye husababisha kujifunza kwa nguvu zaidi na urekebishaji ulioboreshwa.

KIPENGELE CHA 6 – KUREKODI MAREKEBISHO

Unapofanya marekebisho, hakikisha umerekodi mabadiliko na uweke rekodi dhahiri za maamuzi na marekebisho. Kuweka rekodi ya marekebisho na sababu za kutekeleza mabadiliko huruhusu timu kukuza mafunzo yaliyopatikana ambayo yanaweza kusaidia katika ubunifu wa shughuli za miradi ya P/CVE katika jamii sawa au kwingineko. Kando na hayo, kurekodi sababu ya msingi na mchakato wa kutoa maamuzi kuhusu marekebisho ni zana muhimu ya uwajibikaji unapotoa ripoti kwa wafadhili na kuwasiliana na washirika wa mradi. Hati ya marejeleo ya haraka ya Wakfu wa Asia inatoa mwongozo wa kuweka kumbukumbu marekebisho ya mradi wako.

KIPENGELE CHA 7 – BUNI MPANGO WA MAFUNZO NA MAREKEBISHO

Panga mbinu na njia zako za mafunzo na marekebisho kama sehemu ya mpango unaojumuisha kupanga hati kama vile mpango wa Ufuatiliaji, Utathmini na Mafunzo. Tafadhali tumia karatasi hii kujizoeza kutengeneza mpango wako mwenyewe wa kujifunza na kuzoea. 

KIDOKEZO CHA UTEKELEZAJI

ANDAA AGENDA YA KUJIFUNZA

Zana ya CLA ya USAID inajumuisha sehemu ya Ajenda za Mafunzo yenye mwongozo na kiolezo cha kutengeneza ajenda ya kujifunza.