Utangulizi

Sehemu ifuatayo inatoa mwongozo wa jinsi ya kuanza tathmini yako, ikijumuisha malengo yanayoweza kutarajiwa na maswali elekezi. 

Title
Malengo

Kwa nini ukadiriaji wa shughuli za dhana za itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu (VE) ni muhimu kwa shirika lako?

  • Ili kusaidia kuzuia VE kwa kuboresha uelewa wa mambo yanayochangia itikadi kali 
  • Kufahamisha muundo wa shughuli zinazokusudiwa kuzuia au kukabiliana na VE

MODULI HII ITAKUSAIDIA KUTIMIZA NINI?

  • Bainisha hatua na maswali muhimu ya ukadiriaji   
  • Bainisha uhusiano kati ya ukadiriaji wa shughuli za VE na mpango wa shughuli za VE 
  • Elewa jinsi mapendeleo na hali za awali zinavyoathiri ukadiriaji wa miktadha ya eneo ya shughuli za VE na visababishi pamoja na vigezo vya uthabiti 

TUNAWEZAJE KUPUNGUZA UPENDELEO NA KUTAMBUA SEHEMU FICHE KATIKA UCHANGANUZI WA SHUGHULI ZA VE?

  • Bainisha kinachotutia motisha ya kutekeleza ukadiriaji huu 
  • Bainisha viwango vinavyohitajika vya uchanganuzi (kitaifa, kijamii, mtu binafsi, n.k.) 
  • Kadiria jinsi historia yetu inavyoathiri uchanganuzi wetu kwa kujiuliza: je, dhana kuu tulizo nazo ni zipi na zimejaribiwa? 
  • Bainisha iwapo historia yetu inatufanya tuelewa visivyo kitu chochote. Je, kuna mitazamo tofauti ya kuzingatia?  
  • Bainisha iwapo tunaweza kupunguza madhara yanayoweza kutokea kulingana na jinsi tunavyotekeleza ukadiriaji wetu 
Title
Maswali ya Mwongozo wa Ukadiriaji Wako wa Shughuli za VE
UTANGULIZI WA JINSI YA KUTEKELEZA UKADIRIAJI

Baada ya kufafanua maana ya shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu (VE) katika muktadha wako, yafuatayo ni baadhi ya maswali ya msingi ya kuanzisha ukadiriaji wako. Moduli hii inalenga kusaidia timu yako ya kubuni mradi kuelewa miktadha na visababishi vya mgogoro na shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu na uhusiano wa vipengele hivi, ili kukusaidia ubuni mradi wako.  Miktadha ya shughuli za VE huundwa na uhusiano kati ya malalamiko ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu na uwezo wa kustahimili na wahusika wakuu ambao hushawishi watu na nyenzo kulingana na matakwa yao ili kuendeleza malengo ya kijamii, kisiasa au kiuchumi kupitia matendo ya vurugu yaliyohalalishwa kidhana. Visababishi vya shughuli za VE ni vigezo vinavyoweza kuchangia kuzuka kwa shughuli za VE (vinavyojulikana kama “vigezo vya msukumo”) pamoja na vile ambavyo vinaweza kusababisha watu kushawishika na dhana za itikadi kali au kujiunga na makundi yenye itikadi kali (vinavyojulikana kama “vigezo vya mvuto”).  Ubainishaji wa uwezekano wa kuathiriwa na vigezo vya msukumo dhidi ya urahisi wa kulengwa na mashirika yenye dhana za itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu (VEO) husaidia kutenga hatari na kutambua miundo na wahusika wakuu, kunaweza kuleta athari nzuri kwenye miktadha ya VE.

Moduli hii haitaangazia kuhusu utekelezaji wa ukadiriaji wa msingi kwa ajili ya ufuatiliaji na utathmini, ambao unapatikana katika moduli ya Kufuatilia na Kutathmini.

Kutambua watu wanaoweza kuathiriwa
  • Ni watu gani wanaoweza kuathiriwa zaidi na ushawishi wa dhana za itikadi kali na/au kujiunga kwenye kikundi cha dhana za itikadi kali kwenye maeneo yanayolengwa katika mradi wako?
  • Je, kuna vigezo ambavyo vinachangia watu kuandikishwa na mashirika yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu (VEO) (k.m. umri, jinsia, makazi au maeneo ya asili, kiwango cha elimu, hali ya uchumi wa kijamii, kabila au uhusiano wa kidini)?
Kuelewa Vivutio
  • Ni nini vyanzo na malalamiko gani makuu ambayo yanasababisha wasiwasi au hali (vigezo vya msukumo) ambazo zinaweza kuchangia uwezekano wa kushawishika na dhana za VE?
  • Ni vigezo gani vya mvuto ambavyo vinaweza kuwapa motisha watu au makundi kushiriki katika matendo ya vurugu (kwa sababu ya vigezo hivi vya msukumo)?
    • Vigezo hivi vinatofautianaje kati ya wanaume na wanawake (wavulana na wasichana)?
    • Suala la jinsia linawezaje kuathiri mchakato wa kushawishika na dhana za itikadi kali?
  • Ni vigezo gani kati ya hivi ambavyo vinahusiana zaidi na maeneo yanayolengwa katika mradi wako?
  • Ni mahusiano na miktadha gani ya kikundi ambayo huenda inachangia shughuli za VE?
  • Ni mifumo gani muhimu na mbinu au sera husika ambazo zinaweza kuchangia katika uwezekano wa kushawishika na dhana za VE?
Kuelewa matendo ya VEO na uandikishaji
  • Ni maeneo gani ambapo watu wanaweza kulengwa urahisi na VEO ni gani? VEO yamebuniwa kwa muundo gani na hutekelezaje shughuli zake (mpangilio, ufadhili, mawasiliano, n.k.)?
  • Ni nini kinachoeleweka kuhusu mahali na jinsi ambavyo shughuli ya uandikishaji inavyofanywa kwa sasa?
  • Ni nani ambao ni wahusika wakuu na wahamasishaji muhimu katika mfumo unaohusiana na uandikishaji na kushawishi watu kupitia dhana za itikadi kali?
  • Ni vipengele au sifa gani halisi au zinazokisiwa ambazo VEO zenye ushawishi zinazopatikana katika maeneo yanayolengwa kwenye mradi wako hutoa ili kushawishi watu wanaoweza kujiunga nayo?
Kuelewa mitindo ya tishio la shughuli za VE
  • Je, tishio la shughuli za VE linapungua au linaongezeka katika eneo lengwa, na tishio hilo linabadilika katika muundo, upeo na mbinu zinazotumika?
  • Ni matukio na misukumo gani muhimu ya ndani na nje ambayo inaweza kuchangia katika uwezekano wa kushiriki katika shughuli za VE katika maeneo lengwa kwenye mradi?
  • Ni mabadiliko gani mengine ya kimuktadha – yanayohusiana na mgogoro, usawa wa kijinsia, ujumuishaji wa jamii n.k. – ambayo yanaweza kuchangia uwezekano wa kushiriki katika shughuli za VE?  VEO hutumia au yanawezaje kutumia mabadiliko haya katika mazingira yake ya utendakazi ili kuendeleza malengo yake?
Mazingira ya mradi wa CVE na uthabiti wa jamii
  • Je, kuna sera na mikakati ya serikali iliyowekwa kwa ajili ya mradi wa CVE?
  • Je, serikali ya kitaifa itashiriki katika mradi wetu kuhusu suala hili?
  • Je, mamlaka za serikali za kiwango cha eneo/mkoa zitakubali kushiriki katika mradi wetu kuhusu suala hili? Je, zinachukulia suala la shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu kuwa tatizo, na zinachukulia kuwa asasi za kiraia zina jukumu la kutekeleza katika kushughulikia suala hili?
  • Je, kutakuwa na matatizo ya kiusalama kwa shirika kama letu katika kushughulikia kwa uwazi tatizo lashughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu?
  • Ni vigezo gani (watu, mashirika, desturi za kitamaduni, mifumo ya imani n.k.) ambavyo vinaweza kutumiwa kuzuia, kupunguza na kukatiza shughuli za VE katika jamii fulani?
  • Ni nani ambao ni washawishi wakuu (wabaya na wazuri) wanaohusika na kukabiliana na kuzuia shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu katika maeneo yako unayolenga?
  • Ni mafunzo gani yaliyopatikana kutokana na mipango ya awali au ya sasa ya CVE ambayo yanaweza kusaidia kubuni miradi ya siku za usoni ya CVE?

VIDOKEZO VYA UTEKELEZAJI

Utekelezaji wa shughuli za ukadiriaji mara nyingi huwa na hatari sawa kama za utekelezaji wa mradi. Kwa hivyo, unapowazia kuhusu utekelezaji wa shughuli za ukadiriaji, ni muhimu:

  • Kuzingatia hatari zinazokukabili na utumie mbinu ya uzingatiaji wa mgogoro ili usihatarishe maisha yako au maisha ya watu wanaoshiriki katika mradi. Pata maelezo zaidi kwenye Sehemu ya Jumla kuhusu Uzingatiaji wa Mgogoro.
  • Tambua dhana zako ili uwasilishe uchanganuzi wako kwa uwazi.

Shughuli za VE na mgogoro huathiri watu na makundi kwa njia tofauti sana. Kwa hivyo, ni muhimu kuwazia kuhusu mikakati ya ushirikishaji wa wadau ili upate mitazamo na maoni mbalimbali kwenye kazi yako. Kabla ya kutekeleza shughuli ya ukadiriaji, zingatia kuhusu:

  • Jinsi ya kushirikisha vijana kwa ufanisi. Mara nyingi, vijana ni kikundi muhimu kinacholengwa katika miradi ya P/CVE. Kushiriki kwao katika awamu zote za hatua za mradi ni muhimu hasa, lakini pia kuna changamoto. Mfumo wa Ukuaji Bora wa Vijana (PYD) hutoa mikakati muhimu na vidokezo vya utekelezaji. Pata maelezo zaidi kuhusu PYD kwenye Sehemu ya Jumla kuhusu Ushirikishaji wa Vijana.
  • Jinsi ya kujumuisha suala la tofauti ndogo za uelewaji wa jinsia. Mifumo ya ukadiriaji inayoangaziwa kwenye moduli hii yote itakusaidia kutofautisha uchanganuzi wako kulingana na vikundi tofauti vya watu, ikijumuisha wanaume na wanawake. Sehemu ya Jumla kwenye ukurasa wa Jinsia na Ujumuishaji wa Jamii inatoa pia mikakati muhimu na vidokezo vya utekelezaji kuhusu jinsi ya kushirikisha makundi tofauti ya kijamii.