Jedwali la mfumo wa kupanga vipengele muhimu vya mradi na uhusiano wake

Jedwali la Mfumo wa Kupanga Vipengele Muhimu vya Mradi na Uhusiano Wake (LogFrame) ni zana ya ubunifu wa mpango ambayo inaweza kusaidia kuwasilisha Nadharia yako ya Mabadiliko, malengo, makusudi na shughuli zilizobainishwa kwenye Moduli ya Kubuni. LogFrame hutoa mwelekeo wa mradi na husaidia kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa mradi, wafadhili na washirika na wanufaishwa wanaelewa kwa usawa malengo na makusudi ya mradi. LogFrame na mpango wa Ufuatiliaji na Utathmini (M&E) vinapaswa kuwa na uwezo wa kubadilishwa na kukaguliwa mara kwa mara. Kwa kuendelea kukagua hati hizi mara kwa mara katika hatua zote za mradi, unaweza kuhakikisha kuwa zinaonyesha miktadha na malengo yanayobadilika. 

Jedwali la Mfumo wa Kupanga Vipengele Muhimu vya Mradi na Uhusiano Wake (Log Frame) hufafanua:

  • Shughuli za mradi ​
  • Malengo ya muda mfupi na muda mrefu ya mradi ​
  • Jinsi hatua zinazopigwa katika kutimiza malengo zitakavyotathminiwa ​
  • Hatari na dhana ambazo zinaweza kukuzuia kutimiza malengo yako  

How to use the LogFrame

 

logframe1

LogFrame

Unapaswa kusoma safu wima ya muhtasari wa mradi (maelezo) ya LogFrame kuanzia chini hadi juu:

  • Mihtasari iliyoandikiwa vizuri hufuatana kimantiki kwenda juu
  • Kila kiwango cha LogFrame  husababisha kiwango cha juu kinachofuatia
  • Kauli za “ikiwa” na “basi"

Shughuli ni vitendo au matukio ambayo mradi hutekeleza ili kutimiza malengo yake.

  • Kwa mfano: toa mafunzo ya maarifa ya maisha kwa vijana walio katika hatari ya kuathiriwa

Bidhaa au huduma ni bidhaa au huduma halisi zinazotolewa na mradi wako. Mara nyingi huwa rahisi kuhesabika.

  • Kwa mfano: idadi ya vijana walio katika hatari ya kuathiriwa waliopokea mafunzo

Matokeo ni athari nzuri za mradi wako. Hizi zinaweza kuwa za kudumu, kama vile matokeo ya kiwango cha mfumo au kijamii, au ya muda mfupi, kama vile athari za papo hapo za mradi kuhusu mafunzo ya ujuzi au kubadilisha tabia.

  • Kwa mfano: washiriki wanaonyesha tabia na mitazamo bora zaidi

Lengo ni mabadiliko makubwa mazuri ambayo unatarajia kuwa mradi wako utasababisha ulimwenguni.

  • Kwa mfano: kupungua kwa visa vya shughuli za VE