Udumishaji

Mashirika ya eneo mara nyingi hufanya kazi na ufadhili mdogo kiasi na/au ufadhili wa muda mfupi. Hasa miradi ya P/CVE ndio huathiriwa na suala la kupata ufadhili mdogo na wa muda mfupi kwa sababu miradi hii inahitaji ushirikishaji wa kudumu na mpango wa muda mrefu ili kushughulikia visababishi changamano vya shughuli za VE. Kwa hivyo, zingatia kutumia mikakati tofauti ya kujiendeleza unapoweka mpango wa mradi wako wa P/CVE wakati wa awamu ya Kukadiria na katika mchakato wote wa utekelezaji.

UDUMISHAJI UNAMAANISHA NINI?

Katika muktadha wa kazi yetu, kwa kawaida udumishaji huzingatiwa katika viwango vitatu tofauti:

MATOKEO

Results - What does it mean graphic

INAMAANISHA NINI?

Hata baada ya shughuli za mradi kukoma, mara nyingi bado shughuli hizi zinaweza kuwa na athari. Kwa mfano, shirika linalokamilisha mradi wa mafunzo huenda lisiweze kutoa mafunzo kwa watu wageni, lakini washiriki wote waliopokea mafunzo wakati wa mradi wanaweza kuendelea kutumia ujuzi na maarifa yao.

Results - How can you advance it graphic

UNAWEZAJE KUYADUMISHA?

Muundo wa mradi unaweza kuchangia katika udumishaji wa matokeo yake:

  1. Tafuta nyenzo muhimu za ufadhili wa kifedha za kuchukua nafasi ya zile ambazo muda wake wa ufadhili unakaribia kuisha. Kuweka mpango wa udumishaji wa ufadhili wa shughuli fulani unapaswa kuanza wakati wa kubuni shughuli hiyo ili kuhakikisha kuwa shirika linaweza kutambua na kufuatilia nyenzo nyingine za ufadhili. Shirika linaweza kuunda ushirikiano wakati wa utekelezaji wa mradi na mashirika mengine ambayo yanaweza kutoa usaidizi wa kifedha au usio wa kifedha. Kwa mfano, kwa kutumia klabu ya upigaji picha, shirika linaweza kushirikiana na mpango wa kurekodi video wa chuo kikuu ili kupata uwezo wa kufikia vifaa na kushirikisha wanafunzi wa kujitolea ili kutoa ushauri na mafunzo kwa vijana wanaoshiriki katika klabu hiyo.
  2. Ukuzaji wa uwezo ili kuhakikisha kwamba wanaohusika katika udumishaji wa shughuli wana ujuzi wa kiufundi na usimamizi unaohitajika. Kwa kutumia mfano huo, shirika linaweza kuwafunza walimu katika kituo cha vijana ili waendelee kufunza vijana wanaoshiriki katika klabu hiyo.

SHUGHULI

Activities - What does it mean graphic

INAMAANISHA NINI?

Udumishaji wa shughuli za mradi inaweza kumaanisha kuendeleza shughuli zinazofadhiliwa chini ya mradi, kutekeleza shughuli hizo katika maeneo ya ziada na/au kutekeleza shughuli za ufuatiliaji zinazofaa. Kwa mfano, ikiwa mradi unatoa msaada kwa kituo cha vijana ili kuanzisha klabu ya upigaji picha, basi udumishaji wa shughuli za mpango inaweza kumaanisha kuwa klabu inaweza kuendelea kuhudumu na kushirikisha vijana zaidi katika upigaji picha.

Activities - How can you advance it graphic

UNAWEZAJE KUZIDUMISHA?

Shughuli za mradi zinaweza kudumishwa kupitia:

  1. Kutafuta nyenzo muhimu za ufadhili za kuchukua nafasi ya zile ambazo muda wake wa ufadhili unakaribia kuisha kwa kutafuta na kupata nyenzo nyingine za ufadhili. Kuweka mpango wa udumishaji wa ufadhili wa shughuli fulani unapaswa kuanza wakati wa kubuni shughuli hiyo ili kuhakikisha kuwa muundo na utekelezaji wa shughuli hiyo unawezesha shirika kubainisha na kufuatilia nyenzo nyingine za ufadhili. Shirika linaweza kuunda ushirikiano wakati wa utekelezaji wa mradi na mashirika mengine ambayo yanaweza kutoa usaidizi wa kifedha au usio wa kifedha. Kwa mfano, kwa kutumia klabu ya upigaji picha, shirika linaweza kushirikiana na mpango wa kurekodi video wa chuo kikuu ili kupata uwezo wa kufikia vifaa na wanafunzi wa kujitolea ili kutoa ushauri na mafunzo kwa vijana wanaoshiriki katika klabu hiyo.
  2. Ukuzaji wa uwezo ili kuhakikisha kwamba wanaohusika katika udumishaji wa shughuli wana ujuzi wa kiufundi na usimamizi unaohitajika ili kuendelea kutoa huduma husika. Kwa kutumia mfano huo, shirika linaweza kuwafunza walimu katika kituo cha vijana ili waendelee kufunza vijana wanaoshiriki katika klabu hiyo.

VITEKELEZAJI

Implementers - What does it mean graphic

INAMAANISHA NINI?

Hii inamaanisha uwezo wa shirika wa kuendelea kuhudumu na kutekeleza shughuli nyingine siku za usoni. Kwa mfano, shirika lina nyenzo za kifedha na uwezo wa kishirika unaohitajika ili kudumisha kazi yake.

Implementers - How can you advance it graphic

UNAWEZAJE KUVIDUMISHA?

Udumishaji wa shirika unaweza kujumuisha uwekezaji katika:

  1. Udumishaji wa nyenzo za kifedha na uwezo wa kupata ufadhili wa siku za usoni, ikijumuisha uwezo wa kuwa na vyanzo mbalimbali vya ufadhili
  2. Ukuzaji wa uwezo wa shirika wa kukuza ujuzi wake wa kiufundi ili kuweza kutoa mipango bunifu na fanisi, na kwa wasimamizi wa miradi kuhakikisha kuwa wanaweza kufuatilia jinsi huduma zao zinavyohitajika, kutambua na kushughulikia hali zinazobadilika, na kukuza ushirikiano unaofaa

Ukadiriaji wa kishirika unaweza kuwa muhimu sana kwa shirika kutambua mahitaji ya uwezo na kubuni mpango wa kushughulikia mahitaji haya. Tafadhali rejelea Kidokezo cha Utekelezaji kilicho hapa chini.

KIDOKEZO CHA UTEKELEZAJI

ZANA ZA KUKADIRIA UWEZO

Je, ungependa kukadiria uwezo wa shirika lako katika sehemu saba kuu za utendakazi – ikijumuisha uongozi, usimamizi wa rasilimali watu na usimamizi wa fedha? Rejelea zana ya Ukadiriaji wa Uwezo wa Shirika.

Ungependa kukuza uwezo wa kiufundi wa shirika lako katika kubuni mipango ya vijana? Rejelea Zana ya Ukadiriaji wa Mpango wa Vijana ambayo inaruhusu mashirika kukadiria desturi zake za ndani za ubunifu wa mpango na za kimfumo ili kuweza kutekeleza kanuni ya Ukuaji Bora wa Vijana (PYD) kwa lengo kuu la kuboresha ubunifu wa mpango ili kuimarisha matokeo ya ukuaji wa vijana.

UNAWEZAJE KUENDELEZA UDUMISHAJI KATIKA HATUA ZOTE ZA MRADI?

KADIRIA

Tambua shughuli zilizopo ambazo mradi wako unaweza kuendeleza au washirika ambao unaweza kushirikisha.

BUNI

Jumuisha mpango wa ukuzaji wa uwezo au ubunifu wa mpango kwa kushirikiana na jamii wa udumishaji wa shughuli katika muundo wa mradi wako.

TEKELEZA

Shirikisha wadau wa jamii katika utekelezaji wa miradi ya kuendeleza umiliki wa masuala ya eneo.

MAFUNZO

Tambua mafunzo kutokana na ubunifu wa mpango ambayo unaweza kushiriki na wengine ili kudumisha na kupanua matokeo ya mradi wa P/CVE.

KUFUATILIA NA KUTATHMINI

Rekodi matokeo ya mradi wa P/CVE ya kuonyesha athari nzuri za shughuli zako na uweke mpango wa kutafuta ufadhili wa ziada wa kuendeleza miradi yako ya P/CVE.

KWA NINI UDUMISHAJI NI MUHIMU KATIKA MIRADI YA P/CVE?

Suala la shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu ni suala changamano, na visababishi vya shughuli za VE kwa kawaida haviwezi kushughulikiwa kupitia shughuli au mradi mmoja pekee. Kudumisha ushirikishaji na kubuni mipango inayofaa kwa kipindi kirefu huhitajika mara nyingi ili kuona mabadiliko ya maana katika dhana, mitazamo au tabia katika kiwango cha mtu binafsi au kushughulikia masuala ya kimuundo ambayo yanafanya jamii iwe rahisi kuathiriwa na shughuli za VE. Zaidi ya hayo, miradi ya muda mfupi ambayo haibuniwi na kutekelezwa kwa njia ambayo inahakikisha udumishaji inaweza kuzidisha matatizo au malalamiko yaliyopo bila kutarajia. Kwa mfano, mradi unaoanzisha klabu ya vijana lakini hauna mpango wa jinsi ambavyo shughuli zinaweza kuendelea hata baada ya ufadhili wa mradi kukamilika, unaweza kusababisha madhara wakati ambapo vijana walioshirikishwa na kupata motisha zaidi wanaanza tena kujihisi kama wasiojiweza na wasio na msaada wowote wakati mradi huo wa usaidizi unafungwa.

Hata hivyo, tunapozungumzia miradi ya P/CVE, tunaweza kuangazia viwango viwili vya kwanza vya udumishaji:

  • Udumishaji wa matokeo ili mradi wako, ikijumuisha shughuli za muda mfupi, vibuniwe na kutekelezwa ili kuchangia katika kuleta athari ya kudumu ambayo inaweza kuathiri visababishi changamano
  • Udumishaji wa shughuli ili miradi yoyote inayoanzisha ambayo inaweza kuwa muhimu kuendelea baada ya mradi kukamilika, ibuniwe na kutekelezwa kwa njia ambayo inawezesha udumishaji wake

NINAWEZAJE KUWEZESHA UDUMISHAJI WA SHUGHULI NA/AU MATOKEO YA MRADI?

Hakuna njia au mfumo wa jumla wa kuwezesha udumishaji. Kila mradi lazima ubainishe hatua tofauti zitakazochukuliwa ili kuwezesha udumishaji wa shughuli au matokeo yake.

HATUA YA KUSHIRIKISHA WADAU WA JAMII NA KUUNDA USHIRIKIANO INAWEZA KUWEKA MSINGI WA UDUMISHAJI

Kuna uwezekanao zaidi wa jamii kudumisha shughuli ambazo imeshiriki katika kuzibuni na/au kuzitekeleza, ambazo inahisi kuwa zinashughulikia hitaji ambalo imebainisha na ambazo inahisi kuzimiliki. Zaidi ya hayo, unapobuni na kutekeleza shughuli zako, unaweza kushirikisha wadau na washirika ili kupanga jinsi ambavyo unaweza kuendeleza shughuli hizo baada ya kipindi cha ufadhili wa kwanza kukamilika. Kwa mfano, wanaweza kutoa nafasi, utaalamu, vifaa au fedha za kusaidia kudumisha mradi?

KUSHIRIKIANA NA KUBADILISHANA MAELEZO NA MAFUNZO ILI KUDUMISHA MATOKEO

Ni muhimu kwa shirika lako kurekodi mafunzo linapotekeleza shughuli za mradi wa P/CVE (rejelea Moduli ya Mafunzo ili upate maelezo zaidi kuhusu jukumu la mafunzo katika utekelezaji). Kisha unaweza kushiriki mafunzo haya na maelezo husika na wadau na washirika wengine katika jamii yako. Ubadilishanaji huu wa maelezo unaweza kuchangia katika udumishaji wa shughuli kwa njia mbalimbali, ikijumuisha:

  • Kukusaidia kutambua washirika unaoweza kushirikiana nao ambao wangependa kuunga mkono shughuli yako
  • Kuruhushu wengine kujifunza kutokana na kazi yako na bila shaka kutumia maelezo haya katika kazi yao husika ya mradi wa P/CVE, hivyo basi kuzidisha uwezekano kuwa matokeo yako yatadumishwa
  • Kukuruhusu uonyeshe mashirika mengine, ikijumuisha wafadhili wanaoweza kujitokeza, uzoefu wako katika utekelezaji wa miradi ya P/CVE ili wakuone kama mshirika ambaye wanaweza kushirikiana naye katika miradi ya P/CVE

KUJUMUISHA SHUGHULI ZA UKUZAJI WA UWEZO KWENYE MRADI ILI KUTOA ZANA ZA UDUMISHAJI WA MATOKEO

Ukuzaji wa uwezo ni muhimu katika kuendeleza umiliki na kuhakikisha kwamba maarifa na ujuzi muhimu wa kutekeleza miradi ya P/CVE unaweza kuendelea kutumika katika jamii. Ukuzaji wa uwezo unaweza kuangazia:

  • Kukuza kiwango cha kuelewa shughuli za VE na mradi wa P/CVE kwa wadau wa jamii ili kuwezesha wadau hawa wachangie katika ubunifu na utekelezaji wa miradi fanisi ya P/CVE ambayo inazingatia muktadha wa eneo
  • Kukuza ujuzi maalum wa kiufundi unaohitajika ili kudumisha shughuli iliyoanzishwa na mradi: Kwa kutumia mfano wa klabu ya upigaji picha ili kushirikisha vijana waliotengwa, mradi unaweza kukuza uwezo wa walimu wa kituo cha vijana kuhusu ushirikishaji wa vijana kwa ufanisi, kubuni na kupanga shughuli ya ushirikishaji na upigaji picha, mbinu za kuhakikisha kuwa kituo cha vijana kinaweza kuendelea kushirikisha vijana kupitia klabu hiyo
  • Kuendeleza maarifa ya, na uwezo wa kushughulikia mada ambazo zinaweza kuchangia katika udumishaji wa mradi: Hizi zinaweza kujumuisha uhamasishaji wa makundi ya watu wanaoishi nje ya nchi, kushawishi manispaa, kushirikisha sekta ya kibinafsi, uwekezaji wa fedha katika shughuli mbalimbali, kuweka mipango ya kimkakati, n.k.

KUWEKA KATIKA MAKUNDI, KUPANGA NA KUORODHESHA SHUGHULI ZA KUCHANGIA KATIKA KUDUMISHA USHIRIKISHAJI NA MATOKEO YA KUDUMU

Shirika la Office of Transition Initiatives (OTI) linachukua mbinu ya ziada ya kuweka mpango katika nyanja ya mradi wa CVE. Kulingana na mbinu hii, mradi wa OTI unaweza kutekeleza raundi tofauti za shughuli ndogo za muda mfupi, ukitumia kila shughuli na mfululizo wa shughuli ili kubuni na kuweka mpango wa shughuli inayofuatia. Ingawa mbinu hii itaruhusu kupatikana kwa mafunzo na kufanywa kwa marekebisho katika utekelezaji, inatoa changamoto kuu kwa udumishaji wa mradi: matokeo yanayotokana na uwekezaji mdogo (shughuli) yanawezaje kudumishwa baada ya ufadhili wa shughuli hiyo kukamilika? Uzoefu wa OTI unaonyesha kuwa “tofauti zinazoweza kujitokeza katika ubunifu wa mpango na changamoto kubwa kuu vinaweza kushughulikiwa ikiwa wabunifu wa mpango watafikiria mapema na kimpangilio katika mchakato wote wa kubuni mpango kuhusu jinsi shughuli za wastani kiasi za muda mfupi zinavyoweza kuorodheshwa na kupangwa ili kuendelezana na kusababisha upatikanaji wa matokeo yanayotarajiwa ya mradi wa CVE.” Mbinu hii inaweza kuwa muhimu kwa mashirika ya eneo ya asasi za kiraia ikiwa yanaweza tu kutekeleza miradi ya muda mfupi kwa sababu ya ufadhili mchache lakini yanataka kuhakikisha kuwa matokeo yanayotokana na kila mradi yanachangia katika matokeo ya kudumu zaidi ya mradi wa CVE. Kwa maelezo zaidi kuhusu mbinu ya uwekaji katika makundi, upangaji na uorodheshaji katika shughuli za mradi wa P/CVE, rejelea Zana za Mpango wa CVE ya OTI na Mbinu Bunifu za Kubuni Mpango wa CVE.

KUPATA UFADHILI NA KUFIKIA VYANZO MBALIMBALI VYA UFADHILI WA KUDUMISHA KAZI YA P/CVE

Hata ukichukua hatua zote zinazohitajika katika kuweka mpango wa udumishaji wa kazi yako iliyopo ya mradi wa P/CVE, bado huenda ukahitaji kutafuta ufadhili wa ziada ili kuendeleza au kupanua kazi yako. Zingatia mwongozo ufuatao kuhusu ufadhili:

  • Shirikiana na wahusika wa maendeleo wanashughulikia mradi wa P/CVE. Wahusika hawa wanaweza kujumuisha wafadhili wa kimataifa, mashirika ya maendeleo ya kimataifa, mitandao ya eneo au mashirika ya eneo na ya kitaifa ya asasi za kiraia. Ingawa hakuna orodha kamili ya wahusika orodha hii ya mfano inajumuisha mashirika ambayo yameendeleza ushirikiano na ubadilishanaji wa maelezo kati ya wahusika wa miradi ya P/CVE katika sekta au maeneo mahususi. 
  • Shirikiana na jamii yako ili kudumisha mradi wa P/CVE. Shirika lako linaweza kupata nyenzo kutoka katika jamii yako ili kuendeleza miradi au shughuli za mpango wa P/CVE ambazo zinadumisha matokeo ya mradi wa P/CVE. Nyenzo za jamii zinaweza kujumuisha mawazo, muda, utaalamu wa kiufundi, michango ya pesa taslimu au michango isiyo ya pesa taslimu. Kwa mfano, Uchangishaji wa Pesa kutoka kwa Umma hutumia fursa ya kuongezeka kwa matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kutumia mifumo tofauti ya mtandaoni ili kuwasilisha mawazo, miradi au kampeni kwa wafadhili wanaoweza kujitokeza. Wafadhili hawa wanaweza kuwa katika jamii, wana uhusiano na jamii au wangependa tu kuchangia katika mradi ambao unachangiwa pesa. Kwa maelezo zaidi, rejelea: Mifumo ya Ufadhili wa Maendeleo ya Kudumu ya UNDP –Uchangishaji wa Pesa kutoka kwa Umma