Mwongozo huu unahusu nini?

Mwongozo huu umekusudiwa kuyapa mashirika ya asasi za kiraia ulimwenguni nyenzo za kuendeleza miradi yake ya kuzuia na kukabiliana na shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu (P/CVE).

UMEBUNIWA KWA AJILI YA AKINA NANI?

Mwongozo huu umebuniwa kwa ajili ya mashirika ya eneo na watu wanaofanya kazi katika kiwango cha jamii, eneo na kitaifa katika nchi zao ili kuzuia na kukabiliana na shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu.

UMEBUNIWA KWA NJIA GANI?

Nyenzo zilizorejelewa katika mwongozo huu wote ni sampuli zilizochaguliwa za miongozo iliyochapishwa hivi karibuni na zana zinazolenga kutoa mwongozo halisi kwa watekelezaji wa miradi ya P/CVE.

Je, unautumia kwa

mara ya kwanza?

Je, Tayari Umeanza Kutumia?

Karibu Tena!

Chagua Moduli yako

JISAJILI ili upokee Muhtasari wa Taarifa za Mpango wa CVE

Muhtasari wa Taarifa za Mpango wa CVE ni muhtasari wa kila wiki wa ujumbe wa Twitter unaolenga kukusanya makala, mawazo, utafiti na taarifa mpya zinazohusiana na kuzuia na kukabiliana na shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu. Jisajili hapa ili upokee Muhtasari wa Taarifa za Mpango wa CVE.