Ushirikishaji wa Vijana katika Mpango

Mara nyingi vijana ni kikundi muhimu kinacholengwa katika miradi ya P/CVE. Ikiwa hivyo ndivyo ilivyo, ushirikishaji wa vijana katika utekelezaji wa shughuli ni muhimu sana.

Kabla ya kuzingatia kushirikisha vijana katika utekelezaji wa mradi wako, rejelea Sehemu ya Jumla kuhusu Ushirikishaji wa Vijana. Sehemu hii inakusaidia kufafanua maana ya neno “kijana” katika mradi wako, inatoa maelezo ya msingi kuhusu mbinu ya Ukuaji Bora wa Vijana (PYD) ya kushirikisha vijana kwa ufanisi na inabainisha kwa nini ushirikishaji wa vijana na mbinu ya PYD ni muhimu hasa katika mpango wa P/CVE.

Title
Unapaswa kushirikishaje vijana katika utekelezaji wa mradi?

Wakati wa awamu ya Kubuni, ulifafanua kikundi chako unacholenga na kubainisha makundi ya vijana, iwapo yapo, ya kushirikisha katika shughuli zako. Wakati wa awamu ya Kutekeleza, zingatia maswali yafuatayo ili uhakikishe kwamba unashirikisha vijana kwa ufanisi na kwa njia bora, na kuwa hausababishi madhara yoyote yasiyokusudiwa: 

NI NJIA GANI TOFAUTI ZA KUSHIRIKISHA VIJANA KATIKA UTEKELEZAJI WA MRADI?

Utafiti na mipango ya awali imeonyesha kuwa si muhimu tu kushirikisha vijana kama watu wa kunufaishwa na mradi wako, lakini pia kuwashirikisha katika utekelezaji wa mradi wenyewe. Unapofikiria kuhusu jinsi ya kushirikiana na vijana kwa njia bora, zingatia hatua zifuatazo: 

  • Shauriana na vijana kuhusu malengo, maudhui na muundo wa shughuli wakati wa utekelezaji au kuhusu shughuli za ukadiriaji ambazo zinasaidia katika kubuni mpango wako na utekelezaji (hatari au ukadiriaji wa usalama, ukadiriaji wa kanuni za GESI, n.k.)
  • Tumia rasilimali na ujuzi wa vijana kwa kuwaweka katika timu inayotekeleza shughuli–kama wafanyakazi wa kudumu, watoa huduma za muda mfupi au wafanyakazi wa kujitolea.
  • Shirikiana na mashirika yanayoongozwa na vijana, ikijumuisha uhamasishaji na uteuzi wa vijana wa kushiriki, ili kuwezesha utekelezaji wa shughuli au matukio kwa pamoja au kuongoza vipengele mahususi vya mradi wako.

Unapozingatia jinsi ya kushirikisha vijana katika utekelezaji wa mradi, angalia kidokezo hiki cha mwongozo kuhusu viwango tofauti vya ushirikishaji wa vijana.

FUNZO KUU

Ili mradi wako unufaike zaidi kutokana na kushiriki kwa vijana na kuepuka kusababisha madhara, lazima mradi wako uhakikishe kuwa kushiriki kwa vijana kuna manufaa.

Mashauriano na vijana na mashirika yanayoongozwa na vijana yameonyesha kuwa: “Hali ya kushiriki inahitaji kuhusishwa na hisia ya kupata manufaa na uwezo wa kuchangia katika matokeo, badala ya zoezi la kufanywa bila kujali. […] Motisha na ari ambayo inaweza kuletwa na vijana wengi katika ubunifu wa mpango wa maendeleo na miradi ya PVE inaweza tu kutekwa na kudumishwa ikiwa kuna kiwango cha juu cha uaminifu na imani kwamba kushiriki kwao kutakuwa na maana. Hisia hii ya umiliki imeonekana kuwa muhimu sana kwa ufanisi wa mipango ya upunguzaji wa matukio ya vurugu kwa jumla. […] Kutoaminiana kati ya vijana na wahusika wengine ilikuwa ni mojawapo ya changamoto kubwa zaidi katika hali ya vijana kushiriki kikamilifu katika miradi ya uzuiaji wa shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu. Lazima jamii na watu binafsi waamini kwamba kushiriki kwao kunachukuliwa kwa uzito na kunaweza kuleta mabadiliko ya maana.” 

Chanzo

MRADI WAKO UTASHIRIKISHA VIJANA WA AINA GANI?

Baada ya kutambua makundi lengwa katika awamu ya Kubuni, unaweza kuchunguza kwa kina sifa za vijana ambao ungependa kuwashirikisha katika mradi wako. Zingatia pointi zifuatazo unapobuni kigezo chako cha uteuzi:

  • Unafafanuaje kiwango cha umri wa vijana katika muktadha wako? Ikiwa unashirikisha kiwango pana cha umri wa vijana (kwa mfano umri wa miaka 14 hadi 30), fikiria kuhusu jinsi shughuli zako zinavyopaswa kubuniwa ili kufaa makundi ya umri yanayopatikana katika kiwango hiki. Haifai kushirikisha mtu wa umri wa miaka 14 katika shughuli sawa ambazo unaweza kushirikisha mtu wa umri wa miaka 30. Ili upate maelezo zaidi kuhusu hatua za ukuaji wa vijana na kubuni mpango unaofaa kila hatua, rejelea Sehemu ya Jumla kuhusu Ushirikishaji wa Vijana.
  • Je, utashirikisha vijana wa jinsia tofauti? Unawezaje kushughulikia kwa njia bora suala la usawa wa kijinsia na kuzingatia utofauti wa jinsia katika mradi wako?
  • Je, utashirikisha vijana wenye ulemavu? Ikiwa utawashirikisha, unahitaji kufanya nini ili kuhakikisha kuwa wanafikiwa na kuhakikisha wanashiriki kwa ufanisi katika mradi wako?

UNAPASWA KUBUNI AJE MPANGO WAKO WA KUFIKIA NA KUCHAGUA VIJANA?

Unapopanga na kutekeleza mchakato wako wa kuchagua vijana wa kushiriki katika mradi wako, hakikisha kuwa unaelewa athari za kuchagua baadhi ya vijana na kutochagua wengine. Zingatia kwa makini masuala yaliyo hapa chini unapobuni Mpango wako wa Uhamasishaji na Uteuzi na Mpango wako wa Udhibiti wa Hatari:

MASUALA YANAYOWEZA KUJITOKEZA KUTOKANA NA VIJANA AMBAO HAWAJATEULIWA

Mchakato wako unaweza kutenga vijana ambao hawajateuliwa

MASUALA YANAYOWEZA KUJITOKEZA

Kwa jumla, unapoteua vijana wa kushiriki katika mradi mahususi, unapaswa kushiriki manufaa yake na kujitahidi kadri uwezavyo kufanya vijana wavutiwe kushiriki. Hata hivyo, mara nyingi, si vijana wote walio na nia ya kushiriki wanaweza kuchagualiwa. Katika hali hizi, vijana ambao hawajateuliwa wanaweza kuvunjika moyo na kukosa imani wakati hawawezi kufikia fursa au huduma inayotolewa na mradi. Bila shaka hisia hizi zinaweza kuwa tatizo hasa ikiwa vijana ambao hawajateuliwa wanahisi kuwa mchakato wa uteuzi ulitekelezwa kwa njia isiyo ya haki na uwazi au wanaamini kuwa mapendeleo yalifanywa.

NAMNA UNAVYOWEZA KUSHUGHULIKIA HALI HIYO

  • Hakikisha kuwa mchakato wako wa uteuzi unatekelezwa kwa haki na uwazi na kuwa unaeleza kwa njia dhahiri na ya wazi kuhusu kigezo cha uteuzi, mchakato na matokeo.
  • Panga mapema njia za kushirikisha vijana ambao hawajateuliwa katika shughuli nyingine unazopanga na uhakikishe kuwa unaeleza vijana hao kuhusu fursa hizo. Pia, zingatia kujumuisha vijana ambao hawajateuliwa kwenye fursa au mipango mingine ambayo inatolewa na mashirika yanayoshiriki.
  • Eleza jinsi ambavyo mradi unaweza kunufaisha vijana hata kama hawajateuliwa kushiriki. Kwa mfano, mradi unaweza kutoa maelezo yoyote au kuunda nafasi ambazo zitaweza kufikiwa na vijana katika jamii?
Mchakato wako unaweza kutenga vijana ambao hawajateuliwa

MASUALA YANAYOWEZA KUJITOKEZA

Ikiwa kigezo chako cha uteuzi kinatambua kikundi fulani cha vijana (kulingana na jinsia, eneo, kiwango cha elimu, uhusiano wa kidini au kikabila, n.k.) kama kikundi kinacholengwa, mradi wako hautajumuisha makundi mengine ambayo hayalingani na kigezo kinachotumika. Mara nyingi, hali hii haiwezi kuepukika kwa sababu ya lengo la mradi au nyenzo chache, lakini pia inawezekana kusawazisha hali ya kushiriki kati ya makundi yanayoweza kuathiriwa zaidi na yasiyoweza kuathiriwa zaidi na shughuli za VE. Hata hivyo, shirika lako linapaswa kuelewa hatari zinazohusiana na suala hilo na kubuni mikakati ya kuzishughulikia ili kuepuka kusababisha madhara yasiyotarajiwa ikiwa baadhi ya vijana watahisi kutengwa, na kuhakikisha kuwa mchakato wako wa uteuzi hauzidishi bila kutarajia mitindo iliyopo ya matabaka, utengano na kutojumuishwa katika jami.

NAMNA UNAVYOWEZA KUSHUGHULIKIA HALI HIYO

  • Pata maarifa kutoka kwenye mbinu na zana zinazozingatia mgogoro ili ubainishe miktadha ya mgogoro na mitindo ya kutengwa katika jamii yako na uhakikishe kuwa uhamasishaji na mchakato wako wa uteuzi unapunguza madhara.
  • Zingatia kubuni fursa za vijana walioteuliwa kushirikiana na vijana ambao hawakuteuliwa kupitia mbinu ya mafunzo ya wenyewe kwa wenyewe. Kwa mfano, vijana walioteluliwa wanaweza kufikia kikundi kikubwa cha vijana kwa kuelezea vijana wengine kuhusu matokeo ya kazi yao.
  • Zingatia ikiwa kuna manufaa ya kushirikisha makundi mbalimbali ya vijana katika vipengele fulani vya mradi wako. Kwa mfano, hatua ya kushirikisha vijana kutoka maeneo mbalimbali au makundi tofauti ya kikabila inaweza kusaidia kukuza uhusiano bora ambao unaweza kunufaisha mradi na jamii?

MASUALA YANAYOWEZA KUJITOKEZA KUTOKANA NA VIJANA WALIOTEULIWA

Mchakato wako unaweza kufanya vijana walioteuliwa watengwe na wengine

MASUALA YANAYOWEZA KUJITOKEZA

Mradi wako unaweza kubuniwa ili uangazie jamii au vijana mahususi, hasa jamii, makundi au watu uliotambua kuwa wanaweza kuathiriwa na shughuli za VE. Katika hali ambapo mradi wako unashirikisha vijana mahususi, unaweza kusababisha hatari kwa kuhusisha watu au makundi haya na shughuli za VE, hali ambayo itaendeleza dhana potovu na kufanya watengwe zaidi. Hata kutumia lebo ya vijana “walio katika hatari kuathiriwa” inaweza kufanya watengwe, hasa kwa sababu vijana hawa “walio katika hatari ya kuathiriwa” wanaweza kuchukuliwa vibaya na wanajamii wao, jamii zingine na/au vyombo vya usalama, ambavyo huenda vinawalenga kwa shughuli za kukabiliana na ugaidi. Lebo ya “walio katika hatari ya kuathiriwa” inaweza pia kuathiri vibaya vijana ambao wanaweza kujiona kwamba wanaweza kuathriwa au hawana uwezo, badala ya kujiona kwamba wana uwezo.

NAMNA UNAVYOWEZA KUSHUGHULIKIA HALI HIYO

  • Fikiria kwa makini kuhusu jinsi ya kuwasiliana na vijana. Je, unaweza kuepuka kutumia lebo kama vile “walio katika hatari ya kuathiriwa” au “wanaoweza kuathiriwa”?
  • Ikiwa si tayari sehemu ya muundo wa mradi wako, zingatia kujumuisha mbinu za uwezeshaji kulingana na nyenzo katika mradi wako (angalia "Sehemu ya Jumla kuhusu Ushirikishaji wa Vijana" ili upate maelezo zaidi kuhusu mbinu zinazolingana na nyenzo).
  • Zingatia kutumia mbinu ambayo inakuza uaminifu na haja katika vijana.
Mchakato wako unaweza kuhatarisha vijana walioteuliwa, ikijumuisha usalama wao

MASUALA YANAYOWEZA KUJITOKEZA

Vijana wanaoshiriki katika miradi ya P/CVE wanaweza kuwa katika hatari za kiusalama:

  • Kushiriki kwa vijana katika miradi ya P/CVE kunaweza kuvutia makundi ya vurugu na yenye itikadi kali ambayo yanachukulia miradi hiyo kama tishio.
  • Kama ilivyotajwa, mradi wa P/CVE hulenga watu au makundi yaliyotambuliwa kama “yaliyo katika hatari ya kuathiriwa,” watu au makundi haya yanaweza kulengwa katika shughuli za kukabiliana na ugaidi na vyombo vya serikali na vya usalama. Hatari zinaweza kuwa kubwa sana katika nchi ambako serikali imetumia miradi ya P/CVE au CT kama njia ya kukabiliana na upinzani wa kisiasa, uhuru wa raia na haki za binadamu.

MATOKEO YANAYOWEZA KUJITOKEZA

  • Tena, fikiria kwa makini kuhusu jinsi ya kuwasiliana na vijana na jinsi ya kubuni mradi wako. Je, unaweza kuepuka kutumia lebo kama vile “walio katika hatari ya kuathiriwa” au “wanaoweza kuathiriwa”? Je, hatua ya kutaja mradi kama “P/CVE” inahatarisha washiriki? Ikiwa ndiyo, buni mradi wako kwa njia tofauti.
  • Jumuisha hatari za kiusalama zinazoweza kuwakumba vijana wanaoshiriki katika mipango yako ya Usalama na Ushughulikiaji wa Hatari. Je, unahitaji kuchukua hatua mahususi ili kuhakikisha kuwa maelezo kuhusu vijana wanaoshiriki hayafichuliwi? Eleza vijana wanaoshiriki hatari zilizopo na taratibu na sera husika za usalama zilizowekwa.

 

Jedwali lililo hapo juu linatoa ripoti kadhaa, zikiwemo “Mistari ya Mbele: Vijana walio Mstari wa Mbele katika Kuzuia na Kukabiliana na Misimamo mikali yenye Jeuri” na “Vijana na Nyanja ya Kukabili Misimamo mikali ya Ukatili,” pamoja na uzoefu wa FHI 360 wenyewe kufanya kazi na AZAKi za nchini ambao kuwashirikisha vijana katika miradi ya P/CVE.

KIDOKEZO CHA UTEKELEZAJI

UNAWEZAJE KUTAYARISHA SHIRIKA LAKO ILI LISHIRIKISHE VIJANA KATIKA MPANGO NA MRADI WA P/CVE KWA UFANISI?

Yamefupishwa kutoka kwenye nyenzo ya: Young People and Extremism: A Resource Pack for Youth Workers na Youth and the Field of Countering Violent Extremism

1

UNDA NAFASI SALAMA NA ZINAZOFAA ZA KUSHIRIKISHA VIJANA.

Ni muhimu shirika liwe na nafasi na vifaa vinavyofaa vya kukutana na vijana – iwe ni nafasi halisi au ya mtandaoni, na iwapo shughuli za kufanya na vijana zinafanyika katika majengo yaliyotengwa au barabarani, kupitia mbinu ya kufanya kazi “mahali vijana walipo”. Kinyume na kazi ya vijana inayofanyiwa katika eneo moja, kufanya mahali vijana walipo hufanyika mahali ambapo vijana hukutana – kwa mfano, katika mabustani, maeneo ya umma au mitaani. Manufaa ya mbinu hii, ambayo inaangazia kukutana na vijana kulingana na masharti yao wenyewe, ni kwamba inaweza kuunda fursa za kushirikisha vijana ambao kwa kawaida hawafikii huduma za vijana. Hata hivyo, kufanya kazi mahali vijana walipo ni sehemu inayohitaji utaalamu; inahitaji taratibu na sera za kina kuwekwa ili kuhakikisha kuwa ushirikiano na shughuli za kufanya na vijana zinafaa na ni salama.

2

BUNI MFUMO WA USAIDIZI KWA WAFANYAKAZI WANAOFANYA KAZI MOJA KWA MOJA NA VIJANA WANAOSHUGHULIKIA MADA NYETI KAMA VILE MASUALA YA SHUGHULI ZA MAKUNDI YENYE DHANA ZA ITIKADI KALI.

Huduma ya usaidizi kwa wafanyakazi na watu wa kujitolea, hasa wale wanaoshirikiana moja kwa moja na vijana, ni muhimu ili kuhakikisha uthabiti katika huduma zinazotolewa. Usaidizi huu unaweza kuwa kwa namna ya usimamizi wa ana kwa ana au kikundi cha watoa huduma za vijana kinaweza kuungana ili kuzungumzia changamoto na masuala ibuka na kutambua na kushiriki mafunzo waliyopata. Hatua ya kutenga muda wa usimamizi kwa njia hii huleta manufaa kwa watoa huduma za vijana, mashirika yao na hatimaye vijana wanaoshirikiana nao. Inaweza kuleta hali ya ‘kupumzika’ – fursa ya kutafakari na kujitenga na shughuli za mara kwa mara za kubuni mpango, kuandaa, kuratibu na kuwasilisha shughuli na mipango. Usimamizi pia unaweza kusaidia wafanyakazi kukuza ujuzi wao wa kufikiria na kuchanganua mambo kwa kina, wanapotafakari kuhusu mazungumzo waliyofanya na vijana na kutathmini miradi. Kulingana na uchangamano, unyeti na ukubwa wa suala la shughuli za makundi yenye dhana za itikadi kali (hasa itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu), ni muhimu zaidi kwa watoa huduma za vijana kupata usaidizi wanaohitaji ili kuendelea kufanya kazi hii.

3

WEKA DESTURI NA SERA ZA NDANI ZA KUSHUGHULIKIA MASUALA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.

Mashirika yanayoshirikiana na vijana moja kwa moja yanahitaji kuhakikisha kuwa yana miundo ya ndani inayofaa na sera za kina na taratibu za kushughulikia masuala yanayoweza kujitokeza katika sehemu ya vijana na dhana za itikadi kali. Wafanyakazi wote na watu wa kujitolea wanaohusishwa na shirika lazima wafahamu sera na taratibu hizi. Ingawa ni vigumu kubashiri kila hali ambayo inaweza kutokea, ni muhimu kuhakikisha kuwa kuna njia dhahiri za mawasiliano na kuripoti.

4

HAKIKISHA KUWA UNAFAHAMU SERA NA DESTURI AMBAZO ZINAATHIRI VIJANA KATIKA JAMII YAKO.

Mashirika yanapaswa kufahamu mazingira yake ya sera ya mahali, eneo na kitaifa, hasa kuhusiana na sera zinazoathiri vijana moja kwa moja – katika elimu, biashara, kazi, afya, haki na maendeleo ya kijamii. Ingawa si kila mtoa huduma za vijana atakayekuwa na jukumu mahususi la kutekeleza katika masuala ya utetezi wa haki, wengi wao watakuwa na fursa za kuelezea mahitaji ya vijana na kuangazia njia ambazo sera za kitaifa na eneo zinaweza kubuniwa ili kushughulikia maslahi na mahitaji ya vijana kwa njia bora.

5

KUMBUKA UMUHIMU WA KUSHIRIKIANA NA KUBADILISHANA MAELEZO NA MAFUNZO.

Hatua ya kukutana na watoa huduma wengine wa vijana kutoka mashirika mbalimbali haikuzi tu hali ya kusaidiana lakini pia husababisha kushiriki mafunzo na dhana za kujaribu. Hatua ya kukutana na watoa huduma wanaohudumu katika sehemu nyingine zinazohusiana na masuala ya vijana inaweza kuleta manufaa zaidi – kwa mfano, kushirikiana na watoa huduma za afya, walimu na wakufunzi, viongozi wa kidini, wafanyakazi wa umma, wanasiasa, viongozi wa jamii na polisi. Hatua ya kukuza mahusiano na mawasiliano katika miktadha hii tofauti ya kitaalamu hukusaidia kuomba usaidizi au ushauri unapouhitaji – na kuwa na ufanisi zaidi katika kujitahidi kupata matokeo bora zaidi kwa ajili ya vijana. Mahusiano kama hayo yanaweza pia kuleta ushirikiano mpya – kwa mfano, katika kusaidiana kutekeleza mpango au mradi mpya.

6

ZINGATIA ZAIDI WASIFU WA WANATIMU UNAOCHAGUA ILI KUSHIRIKIANA VIJANA.

Hatua ya kuchagua watu wenye hadhi na mali ili washirikiane na watu waliotengwa katika jamii haifai na inapaswa kuepukwa. Inaweza kuwa vigumu kwa watu wanaotoka katika jamii zinazojiweza kufahamu na kuacha kushikilia misimamo ya kijamii na kitamaduni ambayo wameifuata kuanzia zamani. Ujuzi wa kufikia wasiojiweza katika jamii na maarifa ya athari za kutengwa na kanuni za jinsia ni vipengele muhimu kwa wafanyakazi wanaoshughulikia miradi inayoshirikisha vijana.

UNAWEZAJE KUJUMUISHA MBINU YA UKUAJI BORA WA VIJANA KATIKA UTEKELEZAJI WA MRADI WA P/CVE?

Kufikia hapa, umeshirikisha kikamilifu vijana na/au kujumuisha kanuni za PYD katika awamu za Kukadiria na Kubuni za mradi wako. Hata kama hujafanya hivyo, hujachelewa sana kushirikisha vijana katika utekelezaji wa mradi wako kwa kujumuisha kanuni za PYD. Try this exercise below:

Title
doc
Matriki ya Zoezi la Kusaidia Vijana wa PYD
photo
Details

Matriki ya Zoezi la Kusaidia Vijana wa PYD

Matrix hii ya PYD ya Kuingilia kwa Vijana ambayo tulianzisha katika awamu ya Usanifu inaweza kutumika wakati wa awamu ya Utekelezaji kuunganisha shughuli zinazoendelea/zilizopo na vipengele vya PYD na kuendeleza shughuli zilizorekebishwa au mpya zinazokuza PYD.