Uchunguzi Kifani

Title
Kubuni Shughuli Zinazotokana na Ushahidi, Jumuishi na za Kudumu za Ukuzaji wa Uwezo za Mradi wa P/CVE

Association Tétouani de Iniciativas Laborales (ATIL) liliundwa mwaka wa 1993 na tangu wakati huo, limetekeleza zaidi ya miradi ya 50 ambayo inaendeleza ulinzi wa watoto, elimu ya msingi, mafunzo na ujumuishwaji katika jamii na kazini ili kuzuia kutojumuishwa kwa vijana katika jamii. ATIL linahudumu kimsingi katika jiji la Tétouan, Moroko na linashirikiana na mashirika kadhaa ya asasi za kiraia (CSO), mashirika ya kimataifa, taasisi za umma za eneo na huluki za serikali.

Kwa sababu CSO nchini Moroko mara nyingi hayana uwezo wa kufikia nyenzo za kutekeleza shughuli zinazolenga mradi wa P/CVE, ATIL liliamua kuyapa mashirika ya eneo zana ambayo itayasaidia kubuni na kujumuisha shughuli za mradi wa P/CVE kwenye kazi zake zilizopo. Chini ya mradi wa USAID wa Kukabiliana na Shughuli za Makundi yenye Itikadi Kali Zinazohimiza Matendo ya Vurugu katika eneo la Mashariki ya Kati (CoVE-MENA), ATIL lilipokea usaidizi wa kiufundi kutoka shirika la FHI 360 ili kuboresha na kujaribu zana iliyopo ya kusaidia CSO mengine katika kubuni na kutekeleza shughuli za kijamii na kitamaduni zinazozingatia mradi wa P/CVE.

Uzoefu wa shirika la ATIL wa kufanya kazi na vijana waliotengwa na wanaoweza kuathiriwa uliangazia umuhimu wa kushirikisha wadau wa kuaminika – kama vile shule na miungano ya eneo – ili kusaidia kuhakikisha ushirikiano wa jamii za eneo na kupanua eneo la huduma na athari ya shughuli zake. Pia, shirika la ATIL lilitaka kuhakikisha kuwa zana imebuniwa ili kufaa jamii za eneo ambapo kuna kanuni za kale kuhusu jinsia zinazongatiwa zaidi na ambapo suala la shughuli za VE bado ni suala nyeti. Pia, shirika la ATIL liliajiri mtaalamu wa eneo ili kusimamia mchakato wa kushiriki ili kuboresha zana hiyo. Mchakato huu ulijumuisha:

1
Details

Mazungumzo ya kikundi lengwa na wawakilishi sita tofauti wa CSO la eneo ili kusaidia kukadiria uwezo wa shirika na kutambua mahitaji ya CSO kuhusiana na usaidizi wa kiufundi na ukuzaji wa uwezo wa mradi wa P/CVE

2
Details

Warsha ya Mafunzo ya Wakufunzi kwa wafanyakazi tisa wa shirika la ATIL yaliyoongozwa na mtaalamu wa kiufundi kuhusu kubuni na kutekeleza shughuli za uhamasishaji za kijamii na kitamaduni zinazolenga kuzuia shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu

3
Details

Kubuni zana ya kutumiwa na CSO kuhusu jinsi ya kubuni na kutekeleza shughuli za kijamii na kitamaduni ambazo zinajumuisha mbinu za mradi wa P/CVE, ambayo ilijaribiwa kupitia warsha ya mwisho ya mafunzo iliyoongozwa na wakufunzi wa shirika la ATIL kwa wataalamu 22 kutoka kwenye CSO ya eneo na washirika na wadau wengine wa sekta ya elimu

Shirika la ATIL pia lililenga kushirikisha wadau wengi katika kila hatua ya mradi kwa:

  • Kubuni na kutekeleza mbinu inayotokana na zana ya kufunza wadau wa eneo kuiga na kujumuisha shughuli za mradi wa P/CVE kwenye mipango yao ya kijamii inayotekelezwa kwenye maeneo ya elimu ya umma (maktaba za umma, vituo vya utamaduni na shuleni)
  • Kujumuisha mikakati ya ushirikishaji wa wadau ili kushughulikia hatari za kimuktadha na masuala ya jinsia na ujumuishaji wa jamii; na kubuni mpango wa usambazaji na kushiriki maarifa ili kujaribu uwezekano wa kurekebishwa kwa mbinu hiyo katika miktadha miingine

Shirika la ATIL lilibuni shughuli zake za kuhakikisha kwamba shughuli zinadumishwa baada ya kipindi cha utendaji wa mradi kukamilika kwa:

  • Kuendelea kukadiria uwezo na kuangazia kukuza uwezo wa kiufundi wa CSO ili kuhakikisha kwamba kazi inaweza kuendelea baada ya kipindi cha ufadhili wa kwanza kukamilika
  • Kuboresha uwezo wa wafanyakazi wa shirika la ATIL wa kufunza watekelezaji wengine na wafanyakazi wa CSO kuhusu jinsi ya kutumia zana kubuni na kutekeleza shughuli za kijamii na kitamaduni ambazo zinajumuisha mbinu za mradi wa P/CVE
  • “Kupanga na kuorodhesha” mpango wao kwa kubuni shughuli za ufuatiliaji na (CoVE-MENA na wadau wengine) ambazo zinakuza na kuendelea kuimarisha athari za shughuli ya kwanza ya muda mfupi

Kulingana na muundo wa shughuli inayolenga zana ya kukuza uwezo wa CSO, shirika la ATIL lilipanga na kutekeleza angalau shughuli tatu za ufuatiliaji:

  • Kwa kushirikiana na manispaa ya Tétouan, shirika la ATIL lilianzisha mpango wa mafunzo ya CSO katika eneo la Tétouan ili kuimarisha uwezo wake wa kiufundi katika kubuni mipango ya kijamii na kitamaduni. Shirika la ATIL lilitumia zana kama hati ya marejeleo na kufunza washiriki kuhusu jinsi ya kuitumia, ili waweze kubuni na kutekeleza shughuli katika maeneo ya umma wanakohudumu.
  • Kwa kushirikiana na mpango uliofadhiliwa na shirika la Spanish Cooperation Agency (AECID), ATIL na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Utaalamu (Ministry of Education and Vocational Training) jijini Tétouan lilianzisha mradi wa P/CVE wa wataalamu wa elimu ya umma katika shule na taasisi nyingine za elimu ya umma. Lilibuni shughuli shirikishi ya kuchukua hatua ili kubuni na kutekeleza miradi ya P/CVE, uhamasishaji na shughuli za kijamii na kitamaduni ambazo zinachangia katika miradi ya P/CVE shuleni.
  • Shirika la ATIL lilitekeleza shughuli ya miezi mitano chini ya mpango wa ruzuku ya CoVE-MENA ili kuzuia vijana kushawishika kukubali dhana za itikadi kali. Shughuli hiyo ilijumuisha siku ya utafiti wa wadau wengi kuhusu suala la shughuli za VE katika eneo la Tangier-Tétouan-Al Hoceima na mfululizo wa Mafunzo mawili ya Wakufunzi (ToTs) ya CSO ambayo ni washirika wa CoVE-MENA nchini Aljeria na Tunisia ili kushiriki na kujaribu uwezo wa kurekebishwa kwa mbinu ya mradi wa P/CVE ya shirika la ATIL.