Utangulizi

Moduli hii inatoa mwongozo kuhusu jinsi ya kubuni mradi wako wa P/CVE. 

Title
Malengo

MUUNDO WA MRADI UTASAIDIA SHIRIKA LAKO...

  • Kuunganisha ukadiriaji wako wa shughuli za VE na muundo wa miradi na shughuli za P/CVE
  • Buni mradi wako ili usaidie makundi mbalimbali yaliyoathiriwa na shughuli za VE au yale yanayoweza kushawishika kujiunga na VEO
  • Weka mpango wa kukabiliana na hatari kulingana na unyeti wa mpango wa P/CVE
  • Tumia mbinu zinazozingatia mgogoro na suala la jinsia ili kuhakikisha kuwa husababishi madhara katika jamii na mradi wako
  • Buni mikakati ya kushirikisha watu mbalimbali katika ubunifu wa shughuli na mradi wako

MODULI HII ITAKUSAIDIA...

  • Kubainisha uhusiano kati ya ukadiriaji wa shughuli za VE na ubunifu wa mpango wa P/CVE
  • Kuelewa jinsi ya kubuni Nadharia ya Mabadiliko ya mradi wa P/CVE na malengo ya mradi, ambayo yatasaidia katika kuweka mikakati ya ufuatiliaji na utathmini
  • Kuzuia uwezekano wa kusababisha madhara katika ubunifu wa shughuli zako
  • Kugundua mbinu tofauti za kujumuisha mitazamo tofauti katika ubunifu wa mradi wako
Title
Maswali ya Mwongozo wa Kubuni Mradi wako wa P/CVE

Baada ya kukamilisha ukadiriaji wako wa shughuli za VE, zingatia maswali haya ya msingi ya kuanza kubuni mradi wako wa P/CVE:

  • Nadharia ya Mabadiliko ya mradi wako ni gani: yaani, kwa nini/unafirikiaje kuwa vitendo fulani vitaleta mabadiliko yanayotarajiwa katika mazingira yako? Pata maelezo zaidi kwenye ukurasa unaofuata kuhusu jinsi ya kutunga Nadharia ya Mabadiliko.
  • Shirika lako lina uwezo gani wa kutekeleza mabadiliko haya?
  • Mradi wako utajumuishaje masuala ya jinsia na ujumuishaji wa jamii? Hatuwezi kuchukulia kuwa kinachofaa wanaume (wavulana) kinafaa pia wanawake (wasichana). Malengo ya mradi na mbinu za kutimiza malengo hayo zinapaswa kulingana na ukadiriaji sahihi kuhusu mambo ambayo wanaume na wanawake wanaweza kufanya.
  • Utahakikishaje kuwa mradi wako Hautasababisha Madhara?