Utangulizi

Kufikia sasa katika mradi wako, umekadiria vigezo vikuu ambavyo vinasababisha shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu katika muktadha wako (rejelea Moduli ya Kukadiria ili upate nyenzo na mwongozo) na kubainisha muundo wa mradi wako (rejelea Moduli ya Kubuni ili upate nyenzo na mwongozo). Sasa uko tayari kupanga utekelezaji wa mradi wako. Ili kukusaidia katika mchakato huu, zingatia malengo na maswali ya mwongozo yafuatayo:

Title
Malengo
  • Elewa masuala muhimu ya utekelezaji wa mradi wa P/CVE.
  • Pata maelezo kuhusu zana halisi za kutumia kutekeleza masuala haya muhimu. 
Title
Maswali ya Mwongozo

Maswali haya ya mwongozo yatakusaidia kuzingatia jinsi ya kutekeleza mradi wako wa P/CVE.  

  • Utashirikishaje makundi ya wadau muhimu katika utekelezaji wa mradi wako? 
  • Utajumuishaje vijana moja kwa moja katika utekelezaji wa mradi wako?  
  • Utahakikishaje kuwa mradi wako unajumuisha masuala ya jinsia na unajumuisha makundi yaliyotengwa?  
  • Utahakikishaje kuwa mradi wako “hausababishi madhara” tu lakini pia unashughulikia na kupunguza miktadha ya mgogoro kwa njia bora?  
  • Unawezaje kutambua, kuelewa na kuweka mpango wa kushughulikia hatari zinazoweza kutokea wakati wa utekelezaji wa mradi?  
  • Unawezaje kuweka mpango wa kudumisha matokeo ya mradi wakati wa utekelezaji, pamoja na kupata usaidizi na nyenzo za kudumisha matokeo baada ya kukamilika kwa mradi?