Usawa wa Kijinsia na Ujumuishaji wa Jamii (GESI)

Title
Utangulizi

Jamii za ulimwenguni kote zinameundwa na makundi mbalimbali ya kijamii, ambapo yote yana mahitaji, nyenzo, fursa na changamoto tofauti. Njia moja ya kuhakikisha kuwa jamii hizi tofauti zinaeleweka na kuzingatiwa ni kwa kujumuisha dhana za Usawa wa Kijinsia na Ujumuishaji wa Jamii (GESI) katika miradi ya P/CVE. Shirika la Umoja wa Mataifa linaendelea kusisitiza umuhimu wa dhana za GESI katika mipango ya maendeleo; Malengo ya Maendeleo ya Kudumu yanatambua moja kwa moja masuala ya usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake na ujumuishaji wa jamii kama vipengele vya msingi katika kutimiza lengo la kupunguza umaskini na kudumisha ulimwengu wenye afya zaidi, salama, safi, bora, wa watu walioelimika, wenye umoja, wenye haki na wenye usawa zaidi.

Hapa chini utapata maelezo muhimu kuhusu dhana za GESI na jinsi ya kuzijumuisha katika mipango ya P/CVE.

Title
Usawa wa Kijinsia na Ujumuishaji wa Jamii Inamaanisha Nini?

USAWA WA KIJINSIA INAMAANISHA NINI?

“Usawa wa kijinsia inahusisha kushirikiana na wanaume na wavulana, wanawake na wasichana ili kuleta mabadiliko katika mitazamo, tabia, majukumu na wajibu wao wa nyumbani, kazini na katika jamii. Neno Usawa wa kijinsia lina maana zaidi kuliko utofauti wa idadi ya watu au sheria zilizotungwa; inamaanisha kupanua uhuru na kuboresha ubora wa jumla wa maisha ili usawa upatikane bila kuathiri manufaa ya wanaume au wanawake.” Chanzo

UJUMUISHAJI WA JAMII INAMAANISHA NINI?

“Ujumuishaji wa jamii ni mchakato wa kuboresha masharti ya watu na makundi ili kushiriki katika shughuli za kijamii na mchakato wa kuboresha uwezo, fursa na hadhi ya watu wasio na uwezo kwa msingi wa utambulisho wao ili kushiriki katika shughuli za kijamii.” Chanzo

Kulingana na shirika la World Bank, jamii jumuishi lazima iwe na mifumo, miundo na michakato ambayo inawezesha jamii za eneo ili ziweze kuwajibisha serikali zao. Inahitaji pia makundi yote katika jamii kushiriki, ikijumuisha makundi yaliyotengwa tangu jadi—kama vile wanawake, vijana, wazee, mashoga, wasenge, wanaovutiwa na jinsia zote mbili kimapenzi, wasiojitambulisha na jinsia yao halisi, wakosa jinsia (LGBTI), watu wenye ulemavu, jamii za walio wachache na jamii za asili—katika michakato ya kufanya maamuzi. Chanzo 

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI KUUNGANISHA DHANA ZA GESI KATIKA MIRADI YA P/CVE

Kuelewa mienendo ya GESI, haswa jinsia, ni muhimu katika kuelewa mambo ambayo huchangia tabia mbaya na kuunda mikakati madhubuti ya kuingilia kati. Hapa chini kuna mambo machache muhimu ya GESI ya kukumbuka wakati wa kubuni na kutekeleza miradi ya P/CVE:

1
“.. mwanamke hapaswi kuchukuliwa kuwa mtu hatari sana au mtu asiye hatari [kuliko mwanaume], au mpenda amani sana, mpenda mazungumzo, asiyependa vurugu na mwenye kupenda ushirikiano sana kuliko mwanaume.”

Chanzo

Wanaume na wanawake wote ni wahusika na waathiriwa wa mgogoro na vurugu na miradi ya P/CVE inapaswa kuzingatia hilo.

Kwa kawaida, wanaume huchukuliwa kama watu wachokozi na wanawake kama waathiriwa wasio na hatia wa vurugu na mgogoro. Hata hivyo, utafiti mwingi umefanywa miaka ya hivi majuzi ili kuthibitisha kuwa dhana hizi za jumla si za kweli kila wakati na kwamba badala yake, wanaume na wanawake wanapaswa kuzingatiwa kama wahusika na waathiriwa.

2

Majukumu ya kijinsia na kanuni za jamii kuhusu mambo yanayoweza kufanywa/kutofanywa na wanawake/wasichana zinaweza kuzuia uwezo wao wa kushiriki katika shughuli za mpango.

Katika jamii nyingi ulimwenguni kote, kanuni za kidini na kitamaduni zinaweza kudhibiti majukumu ya wanawake na wasichana katika jamii na aina za uhusiano unaoruhusiwa kati ya wanaume na wanawake. Kanuni hizi zinapaswa kuzingatiwa na kusaidia kufahamu jinsi ya kushirikisha washiriki wanawake katika shughuli za mpango. Kwa mfano, majukumu ya nyumbani ya wanawake/wasichana yanaweza kuwazuia kushiriki katika shughuli za mpango. Majukumu ya nyumbani mara nyingi hupewa kipaumbele na kuacha wanajamii wanawake na muda mchache wa ziada wa kushiriki katika shughuli za nje ya nyumbani.

3

Kanuni za kijamii kuhusu uume zinaweza kuathiri iwapo/jinsi wavulana/wanaume wanavyochukulia na/au kushiriki katika shughuli za mpango.

Kama vile tu kanuni za kijamii na za kitamaduni kuhusu wanawake zinavyoweza kuwa vizuizi vya kushiriki kwa mshiriki, kanuni kuhusu uume zinaweza kuwa kizuizi pia. Katika jamii zinazoongozwa na wanaume, wanaume wanachukuliwa kama wanajamii wenye uwezo zaidi katika kitengo cha familia. Ndio wanaotafutia familia zao na pia hulinda na kudumisha heshima ya familia zao. Kwa hivyo, panaweza pia kuwa na changamoto za kushirikisha washiriki wanaume. Huenda wakawa na shughuli nyingi za kutafutia familia zao au kushiriki katika shughuli zingine zinazohusiana na wanaume.

4
“... kwa sababu ya misingi yake ya eneo na wasifu mbalimbali, shughuli za uzuiaji zinazofanywa na wanawake na mashirika ya wanawake zinaaminiwa kuwa na manufaa maalum zinapokuza hali ya uthabiti katika kiwango cha jamii.”

Chanzo

Wanawake wanaweza kutumiwa kama vyombo vyenye ushawishi wa kiwango cha juu vya kuleta mabadiliko na amani katika jamii zao na wanapaswa kushauriwa wakati wa kubuni na kutekeleza mipango ya P/CVE.

Ingawa mara nyingi wanawake huchukuliwa kuwa wapenda amani zaidi kuliko wanaume, dhana hii si ya kweli kila wakati. Wanawake wana kipawa chao mahususi cha kutumika kama wapatanishi na mara nyingi wana kiwango cha juu cha uwezo wa kuhusiana na wanaweza kushawishi kupatikana kwa mabadiliko mazuri katika jamii zao. Katika majukumu yao kama wake, akina mama, akina dada, walezi, viongozi wa jamii, n.k., mara nyingi wanawake wana fursa nzuri ya kutambua dalili za kushawishika na dhana za itikadi kali katika familia na jamii zao, na muhimu zaidi kujaribu kubadilisha hali hiyo. Wanawake wanaweza pia kutumika kama vielelezo vizuri kwa wanaowatunza na kuendeleza kanuni za kuwa na kiasi, ustahimilivu na kukubali.

Pia, mashirika ya wanawake yanaweza kuwa wadau wenye ushawishi wa miradi ya P/CVE. Mashirika haya hayana tu ufahamu muhimu, lakini mara nyingi yana mahusiano ya kina na ya maana katika jamii zao na rekodi nzuri za kushughulikia mahitaji ya jamii.

5
“Suala la jinsia halijitegemei kutoka kwenye vigezo vingine vya kijamii. Suala la jinsia katika mipango ya PVE linapaswa kuchukuliwa kuwa linahusiana na linaingiliana na vigezo vingine kama vile umri, uwezo/ulemavu, hadhi, eneo na hali ya ndoa.”

Chanzo

Jinsia ni Zaidi ya Kuzingatia Wanawake tu

Kulingana na shirika la UNDP and International Alert, “Sehemu kubwa ya suala la uzingatiaji wa jinsia katika mipango ya PVE hulenga majukumu ya wanawake na hali ya kushiriki katika miradi ya PVE.” Hata hivyo, “Inaweza kuwa muhimu zaidi kuchukulia jinsia kama mfumo wa uchanganuzi ambao unajumuisha watu wote: wanawake, wasichana, wanaume, wavulana na watu wasiojitambulisha kama wanaume au wanawake au wanaojitambulisha na jinsia zote mbili. Zingatia jinsi wanawake, wanaume, wavulana, wasichana na watu tofauti wanaojitambulisha na jinsia nyingine wanavyochukulia maisha katika njia tofauti kulingana na, kwa mfano, umri, msingi wa hadhi, hali za maisha, ulemavu au kiwango chao cha elimu.”

Title
Kuanza: Jinsi ya Kuunganisha GESI kwenye Mradi wako

Iwapo unashangaa jinsi ya kuanza kuunganisha dhana za GESI katika mradi wako, anza na Karatasi ya Kudanganya ya Usawa wa Jinsia na Ushirikishwaji wa Kijamii, ambayo inajumuisha maelezo ya kukusaidia kuelewa mahitaji ya GESI kwa mradi wako na hatua za awali za kuchukua. Kwa maelezo zaidi yaliyobainishwa kuhusu jinsi ya kujumuisha dhana za GESI katika mradi wako, tafadhali rejelea moduli za awamu ya mradi mahususi – Tathmini, Sanifu, Tekeleza, Kufuatilia na Katathmini, na Jifunze. Nyenzo za ziada za GESI zimeorodheshwa hapa chini.

Title
doc
ZOEZI LA USAWA WA KIJINSIA NA UJUMUISHO WA KIJAMII