Utangulizi

Title
Malengo

Kufikia hapa katika mradi wako: 

  1. Umekadiria vigezo vikuu ambavyo husababisha shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu katika muktadha wako. Rejelea Moduli ya Kukadiria ili upate nyenzo na mwongozo kuhusu awamu hii ya hatua ya mradi.
  2. Bainisha muundo wa mradi wako, ikijumuisha mbinu na shughuli zako. Rejelea Moduli ya Kubuni ili upate nyenzo na mwongozo kuhusu awamu hii ya hatua ya mradi.
  3. Umeanza kutekeleza shughuli. Rejelea Moduli ya Kutekeleza ili upate nyenzo na mwongozo kuhusu awamu hii ya hatua ya mradi.

Zana na vidokezo vilivyojumuishwa kwenye moduli hii vinapaswa kuzingatiwa katika moduli zote tatu za awali ili kuzingatia jinsi ambavyo unaweza kutathmini kiwango cha athari ya mradi wako. Wakati wa utekelezaji wa mradi, ni muhimu kufuatilia ili kuona iwapo shughuli zako zinachangia katika kutimiza malengo na dhamira yako. Kukusanya data sahihi ya kuonyesha iwapo unapiga hatua ni muhimu. Kwa kawaida wafadhili hawahitaji uripoti tu data hii, lakini mafunzo unayotoa wakati wa utekelezaji wa mradi yatasaidia timu yako kufanya maamuzi bora na kuingiliana na miktadha mipya.

Moduli hii itakusaidia:

  • Kubainisha matokeo ya shughuli zilizopangwa (idadi ya bidhaa na huduma) na matokeo yake (athari nzuri za mradi wako)
  • Kuelewa zana mbalimbali za ukusanyaji na uthibitishaji wa data, ikijumuisha zile ambazo ni muhimu zaidi katika muktadha wa mradi wa P/CVE  
  • Kudhibiti data kwa njia inayozingatia mgogoro  
  • Kutambua mikakati ya utathmini ya kukusaidia kupata matokeo unayotarajia 

Wakati wa kutekeleza shughuli na miradi ya P/CVE, mashirika yanapaswa kujumuisha mbinu za ufuatiliaji na utathmini ambazo zinazingatia vigezo vifuatavyo: 

  • Shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu hubadilika kwa haraka na inahitaji mpango uwe na uwezo kubadilishwa na kurekebishwa  
  • Shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu hubuniwa mahususi ili kufaa kila mazingira ambako zinatendeka, kwa hivyo ni muhimu kutengeneza mafunzo ya kusaidia kuleta mabadiliko yoyote kwenye shughuli za mradi 
  • Shughuli za ufuatiliaji na utathmini (kama vile ukusanyaji wa data) lazima zifanywe kwa njia inayozingatia mgogoro 
Title
Maswali ya Mwongozo

Unapoanza kubuni na kutekeleza mradi wako, zingatia kuhusu jinsi unavyoweza kutathmini mafanikio yake. Unapobuni na kutekeleza mpango wa ufuatiliaji na utathmini wa mradi wako, zingatia maswali haya: 

KUBUNI

  • Kwa nini umechagua shughuli hizi mahususi? 
  • Ungependa shughuli zako zitimize malengo gani? 

KUTEKELEZA

  • Je, mradi wako unatumia pesa na nyenzo kwa njia inayofaa?
  • Je, matatizo yoyote yamejitokeza?
  • Je, umetambua mafanikio yoyote?
  • Je, mradi wako unatimiza malengo yake? 
  • Je, unafuatilia muktadha mara kwa mara ili kuhakikisha mradi unaendana na mazingira ya sasa? 
  • Je, washiriki wako hatarini iwapo wahusika fulani watapata majina na majibu yao baada ya kukusanya data? 
  • Je, unadhibiti vipi mawasiliano ya taarifa na data nyeti? 

MAFUNZO

  • Je, kuna kitu kilichotokea ambacho hukukipangia?​ 
  • Je, ulitambua kitu ambacho hakikutarajiwa?​ 
  • Kulingana na ulichojifunza, ni marekebisho gani unahitaji kufanya kwenye shughuli zako? 
Title
Utangulizi kuhusu Dhana za Ufuatiliaji na Utathmini (M&E)

Ufuatiliaji na utathmini ni maneno ambayo mara nyingi hutajwa pamoja lakini yanapaswa kueleweka kama dhana tofauti:

Ufuatiliaji: Ukusanyaji wa data katika mchakato wote wa utekelezaji wa mradi ili kubaini iwapo mradi unatimiza malengo yake, unatumia pesa na nyenzo kwa njia inayofaa na kurekebishwa panapohitajika.

Utathmini: Ukadiriaji wa mradi ili kubaini ufanisi na athari zake.

Shughuli zote mbili za ufuatiliaji na utathmini zinapaswa kusaidia shirika kubaini iwapo mabadiliko yanahitaji kufanywa kwenye mradi wa sasa au shughuli za baadaye za mradi. Moduli ya Mafunzo itakupa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia data iliyokusanywa ili kuboresha mpango wako.

  Hufanywa mara ngapi? Hujibu maswali ya aina gani? Aina gani ya data ambayo hutumika? Hufanywa na nani?
UFUATILIAJI Mara kwa mara, kila siku, kila wiki na/au kila mwezi
  • Je, mradi wako unatimiza malengo yake?
  • Je, mradi wako unatumia pesa na nyenzo kwa njia inayofaa?
  • Je, matatizo yoyote yamejitokeza?
  • Je, umetambua mafanikio yoyote?
Data kuhusu shughuli, matumizi ya pesa na matokeo ya muda mfupi Mwanatimu yeyote anayehusika katika mradi
UTATHMINI

Wakati maalum

Kwa mfano: katikati ya mradi, mwisho wa mradi au mwisho wa mwaka

  • Je, mradi wako ulitimiza malengo uliotarajia kutimiza?
  • Je, mradi wako ulitumia pesa na nyenzo vizuri?
  • Je, kuna kitu kilichotokea ambacho hukukipangia?
  • Je, ulitambua kitu ambacho hakikutarajiwa?
Data kuhusu matokeo na malengo ya jumla Timu ya utathmini: ya ndani au nje
Title
MPANGO WA UFUATILIAJI NA UTATHMINI (M&E)

Hatua ya kufuatiliaji utendaji wa mradi huruhusu shirika kufuatilia hatua zinazopigwa katika kutimiza malengo na makusudi yake. Ingawa wafadhili hutumia violezo tofauti kupanga maelezo haya, sehemu kuu zinaweza kujumuisha: 

1
Details
Muhtasari wa Mradi
  • Kusudi: Toa maelezo kamili na yanayoeleweka ya kanuni kuu ya mpango wa Ufuatiliaji na Utathmini (M&E) (k.m. nia/kusudi, matumizi ya nyenzo, ushiriki, uwazi, n.k.). 
  • Mfumo wa Matokeo: Onyesha jinsi kazi zilizo kwenye mpango wa kazi zinavyohusiana na viashirio na zinavyofaa kwa kusudi la mradi [au kusudi ndogo]. 
2
Details
Shughuli na Muktadha

Toa maelezo kamili na yanayoeleweka kuhusu muktadha, nadharia ya ubunifu, lengo la mradi, kusudi, eneo lengwa, pamoja na mahali au jinsi shughuli hizi zinavyochangia katika matokeo yanayotarajiwa ya mradi mkubwa.

3
Details
Viashirio vya Utendaji

Viashirikio vinahitajika kwa kila shughuli/malengo ya mradi. Viashirio vinapaswa kujumuisha misingi na malengo, na kila kiashirio kinapaswa kuhusishwa moja kwa moja na matokeo yake. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu viashirio baadaye katika moduli hii.

4
Details
Usimamizi wa Mfumo wa Ufuatiliaji wa Utendaji

Toa maelezo kamili na yanayoeleweka kuhusu miundo ya Ufuatiliaji na Utathmini (M&E) ya shughuli, kazi na uwezo (k.m. ni mfanyakazi yupi aliye na jukumu lipi katika shughuli ya Ufuatiliaji na Utathmini (M&E)). Toa njia za kushughulikia matatizo yaliyobainishwa (k.m. weka mpango wa uimarishaji wa uwezo wa wafanyakazi, ushirikiano na mashirika ya Ufuatiliaji na Utathmini (M&E) ili kuimarisha mfumo wa Ufuatiliaji na Utathmini (M&E), n.k.).

5
Details
Ratiba ya Kutoa Ripoti ya Utendaji

Toa mfumo (chati ya Gantt) unaoonyesha kazi zilizopangwa kutekelezwa, mara za kutekelezwa, muda, watu wanaowajibika n.k. wa ufuatiliaji wa utendaji.

6
Details
Mpango wa Utathmini

Onyesha shughuli za utathmini zilizopangwa na ratiba inayopendekezwa.

7
Details
Hati ya Marejeleo ya Kiashirio cha Utendaji wa Shughuli (PIRS)

Hati ya Marejeleo ya Kiashirio cha Utendaji wa Shughuli (PIRS) ni zana inayotumiwa na shirika la USAID kufafanua viashirio vya utendaji. Ni muhimu katika kuhakikisha uthabiti na ubora wa data ya kiashirio.