Istilahi Muhimu

Neno/Kifupisho   Neno Kamili 
AAR  Ukaguzi wa Baada ya Kitendo (After-Action Review)  
CAF 2.0 Mfumo wa Ukadiriaji wa Mgogoro (Conflict Assessment Framework)
CBO Shirika la Kijamii (Community-Based Organization)
CDA Miradi ya Mafunzo ya Ushirikiano ya CDA (CDA Collaborative Learning Projects)
CGCC Kituo cha Ushirikiano wa Kukabiliana na Ugaidi Ulimwenguni (Center on Global Counterterrorism Cooperation)  
CSOs Mashirika ya Asasi za Kiraia (Civil Society Organizations)
DFID Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (United Kingdom Department for International Development)
FBO Shirika la Kiimani (Faith-Based Organization)
FTFs Wapiganaji wa Kigaidi wa Kigeni (Foreign Terrorist Fighters)
GCCS Kituo cha Kimataifa cha Usalama wa Ushirikiano (Global Center on Cooperative Security) 
GCERF Fedha za Kimataifa za Ushirikishaji na Kukuza Uthabiti wa Jamii (Global Community Engagement and Resilience Fund) 
GCTF Baraza la Kimataifa la Kukabiliana na Ugaidi (Global Counterterrorism Forum)  
GESI Usawa wa Kijinsia na Ujumuishaji wa Jamii (Gender Equality and Social Inclusion)
GLAM Mafunzo ya Kimataifa ya Mpango wa Udhibiti Unaobadilika (Global Learning for Adaptive Management Initiative)
ISO Shirika la Kimataifa la Usawazishaji (International Organization for Standardization)
LGBTI Wasagaji, Wasenge, Wanaovutiwa Kimapenzi na Wanaume na Wanawake, Wasiojitambulisha na Jinsia yao Halisi, Wenye Jinsia Mbili
LogFrame Jedwali la Mfumo wa Kupanga Vipengele Muhimu vya Mradi na Uhusiano Wake
M&E Ufuatiliaji na Utathmini
NGO Shirika Lisilo la Serikali
OTI Ofisi ya Mipango ya Mabadiliko ya Shirika la USAID
P/CVE Kuzuia na Kukabiliana na Shughuli za Makundi yenye Itikadi Kali Zinazohimiza Matendo ya Vurugu
PIRS Hati ya Marejeleo ya Kiashirio cha Utendaji
PQA Ukadiriaji wa Ubora wa Mpango
RAN Mtandao wa Uhamasishaji kuhusu Kushawishika na Dhana za Itikadi Kali 
RESOLVE Mtandao wa Nyenzo za Utafiti kuhusu Visababishi vya Shughuli za Dhana za Itikadi Kali Zinazohimiza Matendo ya Vurugu na Vyanzo vya Uthabiti wa Jamii  
RUSI Taasisi ya Wataalamu wa Ulinzi na Usalama ya Uingereza (Royal United Services Institute)
SMS Huduma ya Ujumbe Mfupi
ToTs Mafunzo ya Wakufunzi
UN Umoja wa Mataifa
UNDP Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa
USAID Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa
USIP Taasisi ya Masuala ya Amani ya Marekani (United States Institute of Peace)

 

 

Neno/Kifupisho Neno Kamili Ufafanuzi
Walio katika hatari ya kuathiriwa  

Walio katika hatari ya kuathiriwa ni kauli inayorejelea watu, makundi au jamii ambazo zinaweza kuathiriwa hasa na tishio la shughuli za VE kwa sababu ya ukaribu au urahisi wao kuathiriwa na miktadha na visababishi vya shughuli za VE.

(umetolewa kutoka kwenye nyenzo mbalimbali)

C-AM Ufuatiliaji Unaozingatia Uchangamano

C-AM ni aina ya ufuatiliaji wa ziada ambao ni muhimu wakati ni vigumu kubashiri matokeo kwa sababu ya miktadha inayobadilika au wakati uhusiano wa sababu na athari si dhahiri. Wakati uwezo wa kubashiriki matokeo na njia za kawaida ni mdogo, data ya ufuatiliaji unaozingatia uchangamano hutoa kiwango kamili cha matokeo, vigezo vya kawaida na njia zinazochagia.

(Chanzo: Discussion Note: Complexity-Aware Monitoring, USAID, 2018)

CLA Kushirikiana, Kujifunza na Kurekebisha

CLA ni mfumo wa shirika la USAID wa utekelezaji wa udhibiti unaobadilika katika hatua za mradi. CLA inajumuisha ushirikiano wa kimkakati na mafunzo endelevu ya udhibiti unaobadilika na hali zinazowezesha michakato hii.

(Chanzo: Discussion Note: Adaptive Management, USAID, 2018)

 

Mshikamano wa Jamii (Umoja wa Kijamii)  

Jamii yenye mshikamano ni jamii ambayo “hujitahidi kuboresha maslahi ya wanajamii wake wote, hupinga hali za ubaguzi na kutengwa, hukuza hisia ya kukubaliwa, hukuza uaminifu na huwapa wanajamii wake fursa ya kustawi na kukua kijamii.”

(Chanzo: OECD)

Mshikamano wa kijamii unahusu kukubali na kuheshimu utofauti (kuhusiana na dini, ukabila, hali ya kiuchumi, misimamo ya kisiasa, mwelekeo wa kijinsia, jinsia na umri)—kwa kiwango cha kimfumo na cha mtu binafsi. Ingawa kuna utata kuhusu maana ya mshikamano wa kijamii, kuna vipimo viwili vikuu vinavyohusishwa nayo: (1) Kupungua kwa hali za utofauti, utofauti wa sawa na kutengwa kijamii. (2) Uimarishaji wa mahusiano ya kijamii, mahusiano na mshikamano.

(Chanzo: UNDP)

Uzingatiaji wa Mgogoro  

Uzingatiaji wa Mgogoro ni kauli inayorejelea hali ya kuelewa jinsi ambavyo miradi ya msaada inahusiana na mgogoro katika muktadha mahususi, kwa lengo la kupunguza athari mbaya zisizotarajiwa na kuleta mabadiliko mazuri kuhusiana na mgogoro panapowezekana, kupitia miradi ya uhisani, maendeleo na/au za kukuza amani.

(Chanzo: CDA)

Viunganishi  

Viunganishi ni vipengele muhimu vya mfumo wa Usisababishe Madhara. Viunganishi ni vyanzo vya mshikamano na uaminifu katika jamii. Viunganishi huonyesha uwezo ambao watu wanao wa kuleta amani na husaidia kuwezesha kuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya watu wanaotofautiana.

(Chanzo: yametolewa kwenye Do No Harm Workshop, Participants Manual, CDA, 2016)

CT Kukabiliana na Ugaidi

Miradi inayolenga kudhibiti, kukomesha na kufuatilia magaidi na shughuli za kigaidi.

(umetolewa kutoka kwenye nyenzo mbalimbali)

CVE Kukabiliana na Shughuli za Makundi yenye Itikadi Kali Zinazohimiza Matendo ya Vurugu

Kukabiliana na Shughuli za Makundi yenye Itikadi Kali Zinazohimiza Matendo ya Vurugu ni kauli inayorejelea hatua za mapema za kuwahi au kukatiza shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu za kushawishi, kuandikisha na kuhamasisha wafuasi wake kutekeleza matendo ya vurugu na kushughulikia vigezo mahususi ambavyo vinachochea watu kujiunga na kushawishika kushiriki katika matendo ya vurugu. Mpango wa CVE unajumuisha sera na shughuli za kuongeza njia za amani za kushughulikia masuala ya kujumuishwa kisiasa, kiuchumi na kijamii zinazopatikana kwa jamii na serikali za eneo na uwezo wao wa kuzitumia.

(Chanzo: Updated from the U.S. Department of State & USAID’s Joint Strategy on Countering Violent Extremism, 2016)

Vitenganishi  

Vitenganishi ni vipengele muhimu vya mfumo wa Usisababishe Madhara. Vitenganishi ni vyanzo vya kuleta hali ya wasiwasi, kutoaminiana au kushukiana katika jamii ambavyo awali vilisababisha au vinaweza kusababisha mgogoro baina ya makundi siku za usoni. Vinazuia kuwepo kwa mahusiano mazuri.

(Chanzo: yametolewa kwenye Do No Harm Workshop, Participants Manual, CDA, 2016)

DNH Usisababishe Madhara

Mbinu ya DNH ni mbinu ya uzingatiaji wa mgogoro ambayo inafaa zaidi kwa miradi inayotekelezwa katika mazingira yenye mgogoro. Mbinu ya DNH inaweza kujumuishwa kwenye hatua nyingi za mradi. Haijabuniwa tu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa miradi yako haizidishi visababishi vya mgogoro au kukuweka wewe, wafanyakazi wako na wanufaishwa katika hatari, lakini imebuniwa pia ili kuhakikisha kuwa mradi wako unachangia katika uzuiaji wa shughuli za dhana za itikadi kali au mgogoro wenye vurugu. Kipengele muhimu cha mfumo wa DNH ni kufanya uchanganuzi wa vitenganishi na viunganishi ambavyo huharibu au kukuza mahusiano kati ya makundi.

(Chanzo: yametolewa kwenye Do No Harm Workshop, Participants Manual, CDA, 2016)

Visababishi vya Shughuli za Makundi yenye Itikadi Kali Zinazohimiza Matendo ya Vurugu  

Vigezo ambavyo vinaweza kuchangia katika kuzuka kwa shughuli za dhana za itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu au uvamizi pamoja na vile ambavyo vinaweza kushawishi watu kukubali dhana za itikadi kali. Visababishi mara nyingi hugawanywa katika vigezo vya msukumo na mvuto.

(Chanzo: Development Response to Violent Extremism and Insurgency, USAID, 2011) 

Usawa wa Kijinsia  

Usawa wa kijinsia unahusisha kushirikiana na wanaume na wavulana, wanawake na wasichana ili kuleta mabadiliko katika mitazamo, tabia, majukumu na wajibu nyumbani, kazini na katika jamii. Kauli ya usawa wa kijinsia ina maana zaidi kuliko utofauti wa idadi au sheria zilizotungwa; inamaanisha kupanua mipaka ya uhuru na kuboresha ubora wa jumla wa maisha ili usawa upatikane bila kuathiri manufaa ya wanaume au wanawake. 

(Chanzo: Gender Equality and Female Empowerment Policy, USAID, 2012)

Hatua za Mradi  

Hatua za  Mradi ni mpangilio na istilahi ya shirika la USAID ya kubainisha kikundi cha kawaida cha michakato inayokusudiwa kufanikisha miradi fanisi zaidi ya maendeleo na kuleta mabadiliko ya kiwango cha juu zaidi. Inajumuisha vipengele vifuatavyo: Ubunifu wa CDCS, ubunifu na utekelezaji wa mradi, udhibiti wa utendaji, utathmini, mafunzo na marekebisho na bajeti na nyenzo. Tumeiga hatua za mradi za Mwongozo huu wa Marejeleo wa Mpango wa CVE ili kurejelea awamu tano zifuatazo za hatua za mradi: (1) Kukadiria, (2) Kubuni, (3) Kutekeleza; (4) Kufuatilia na Kutathmini; na (5) Mafunzo.  

Vigezo vya Mvuto  

Vigezo vya mvuto vinaathiri moja kwa moja kiwango cha mtu binafsi cha kushawishika na dhana za itikadi kali na ni visababishi ambavyo huvutia watu kujiunga na makundi na miungano ya shughuli za VE—kama vile ombi la kiongozi fulani, imam aliyejiteua mwenyewe au mtu mashuhuri au manufaa ya vitu halisi, ya kihisia au ya kiroho ambayo yanaweza kupatikana kwa kujihusisha na kikundi.

(Chanzo: Development Response to Violent Extremism and Insurgency, USAID, 2011)  

Vigezo vya Msukumo  

Vigezo vya msukumo ni sifa za mazingira ya kijamii ambayo hudaiwa kusukuma watu wanaoweza kuathiriwa kujiunga na kutekeleza matendo ya vurugu. Vigezo hivi vya kimfumo vinajumuisha viwango vya juu vya kutengwa kijamii na kugawanywa katika makundi; maeneo yenye uongozi duni au yasiyo na uongozi; kukandamizwa na serikali na ukiukaji wa haki za binadamu; ufisadi uliokithiri na kutoadhibiwa kwa watu wenye mali na hadhi ya juu; na dhana za kudhuriwa na utamaduni wa kigeni.

(Chanzo: Development Response to Violent Extremism and Insurgency, USAID, 2011)

PVE Uzuiaji wa Shughuli za Makundi yenye Itikadi Kali Zinazohimiza Matendo ya Vurugu

Uzuiaji wa shughuli za Makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu haupaswi tu kuangazia masuala ya kuwekwa kwa usalama mkali bali pia unapaswa kuangazia sababu zinazohusiana na maendeleo na suluhu za suala hili. Kwa hivyo, suluhu za kudumu za uzuiaji wa shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu zinahitaji mbinu ya maendeleo jumuishi iliyojikita kwenye msingi wa kuvumiliana, kuwezeshwa kisiasa na kiuchumi na kupungzwa kwa hali za utofauti.

(Chanzo: Preventing Violent Extremism Through Promoting Inclusive Development, Tolerance, and Respect for Diversity, UNDP, 2016)

PYD Ukuaji Bora wa Vijana

PYD ni mbinu inayozingatia suala la ukuaji wa vijana inayoangazia kuongezeka kwa nyenzo za vijana na kuimarisha vigezo vya ulinzi. Mbinu ya PYD hushirikisha vijana pamoja na familia, jamii na/au serikali zao ili vijana wawezeshwe kufikia uwezo wao kamili. Mbuni za PYD hukuza ujuzi, nyenzo na ustadi; hukuza mahusiano bora; huimarisha mazingira; na kubadilisha mifumo.

(Chanzo: Yametolewa kwenye nyenzo ya Promoting Positive Youth Development, YouthPower)

Kushawishika na dhana za itikadi kali  

Kushawishika na dhana za itikadi kali ni mchakato ambapo mtu au kikundi hukubali dhana au itikadi kali na kuona vurugu kama njia halali ya kuziendeleza. Ingawa watu wengi wanaokubali mitazamo yenye itikadi kali hawajihusishi na matendo ya vurugu kamwe, wale ambao hujihusisha na matendo ya vurugu mara nyingi hukubali dhana zinazounga mkono matendo yao.

(Chanzo: Radicalization Revisited: Jihad 4.0 and CVE Programming, USAID, 2016)

Uandikishaji/Kujiunga   

Uandikishaji ni kauli inayorejelea mchakato ambapo watu ambao tayari ni wanachama wa kikundi chenye dhana za itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu huandikisha watu wengine kujiunga nacho. Kiwango ambapo shughuli kama hiyo ya uandikishaji hufanywa kwa njia ya mpangilio na ya kimfumo hutofautiana kutoka hali moja hadi nyingine; katika upande mmoja wa mchakato, uandikishaji wa wanachama kutoka juu hadi chini hufanywa na watu binafsi (“waandikishaji”) ambao wamekabidhiwa jukumu hili hasa na ambao hufanya kazi katika kitengo maalum ambacho kimekabidhiwa kazi hiyo. […] Kwa upande mwingine, “Kujiandikisha mwenyewe,” inarejelea mchakato ambapo watu hujiunga wenyewe kwenye makundi ya [VEO], kwa njia ya moja kwa moja au kupitia mtandaoni; hufanya hivyo kwa kutumia sana sana usaidizi mdogo wa moja kwa moja au mipango ya kimakusudi iliyopangwa na wengine.

(Chanzo: Development Response to Violent Extremism and Insurgency, USAID, 2011)

Uthabiti    

Uthabiti unaweza kuwa katika viwango na miundo tofauti. Kwa hivyo, ufafanuzi wa uthabiti utategemea vigezo vinavyojumuisha kiwango cha usaidizi au huluki unayolenga (mtu binafsi, kikundi au jamii) na aina ya hali unazojaribu kudhibiti (janga la kiasili, ukosefu wa chakula cha kutosha, mgogoro/vurugu, shughuli za dhana za itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu, ugonjwa, n.k.). Kwa jumla, shirika la USAID linafafanua uthabiti kama “uwezo wa watu, familia, jamii, nchi na mifumo wa kushughulikia, kuingiliana na kurejelea hali ya kawaida kutokana na misukosuko na hali za wasiwasi kwa namna ambayo inapunguza uwezekano wa kuathiriwa mara kwa mara na kuwezesha ukuaji jumuishi.”

Udhibiti wa Hatari  

Udhibiti wa hatari ni mbinu ya kimfumo na hali ya kudhibiti hali zisizotabirika ili kupunguza hasara na madhara yanayoweza kutokea na kukuza zaidi fursa na manufaa yanayoweza kupatikana. Lengo la udhibiti wa hatari ni “kuweka utaratibu bora wa hatua za kuchukuliwa chini ya hali zisizotabirika kwa kutambua, kukadiria, kuelewa, kufanya maamuzi na kushughulikia masuala ya hatari.” Udhibiti wa hatari ni mchakato muhimu wa uwezeshaji: kuliko kutoa maamuzi ya kukomesha mpango, michakato fanisi ya udhibiti wa hatari huunda hali zinazohitajika ili mradi uendelee na bila shaka ufaulu.

(Chanzo: Risk Management for Preventing Violent Extremism Programmes: Guidance Note for Practitioners, UNDP, 2018)

Ujumuishaji wa Jamii  

Ujumuishaji wa jamii ni mchakato wa kuboresha masharti ya watu na makundi kushiriki katika jamii na mchakato wa kuboresha uwezo, fursa na hadhi ya watu wasio na uwezo kwa msingi wa utambulisho wao ili kushiriki katika jamii.

(Chanzo: World Bank)

Wadau  

Mshika dau ni mtu, kikundi au shirika lolote ambalo linaathiriwa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na shughuli au mradi utakaotekelezwa. Wadau wanaweza pia kuathiri vibaya au vizuri matokeo ya shughuli/mradi. Mifano ya wadau inajumuisha; watu au jamii za eneo, mamlaka za serikali za eneo na kitaifa; wawakilishi wa asasi za kiraia; mashirika yasiyo ya serikali ya mitaa, eneo, kitaifa na kimataifa; na wenyeji, viongozi wa kidini, wasomi, wawakilishi wa sekta za kibinafsi, mashirika ya Umoja wa Mataifa, wafadhili wa kimataifa na makundi maalum yenye nia ya kushiriki.

(umetolewa kutoka kwenye nyenzo mbalimbali)

Udumishaji  

Katika muktadha wa kazi ya maendeleo, kwa kawaida udumishaji huangaziwa katika viwango vitatu tofauti: (1) udumishaji wa matokeo na athari za shughuli; (2) udumishaji wa shughuli za mradi kupitia kuendelezwa baada ya ufadhili kukamilika, kusambaza shughuli hizo katika maeneo ya ziada na/au kutekeleza shughuli za ufuatiliaji zinazofaa; na (3) udumishaji wa watekelezaji—yaani, uwezo wa shirika wa kuendelea kuhudumu na kutekeleza shughuli zingine siku za usoni.

(Chanzo: Yametolewa kwenye nyenzo ya Incorporating Sustainability Plans into Grant Programs, NGO Tips, Capable Partners Program, USAID and FHI 360, 2011)

ToC Nadharia ya Mabadiliko

ToC ni ufafanuzi wa jinsi na kwa nini kikundi fulani cha shughuli kitasababisha mabadiliko fulani. Hufuata mantiki rahisi ya jumla ya “ikiwa/basi” : yaani, ikiwa shughuli itatekelezwa kwa ufanisi, basi itasababisha matokea yanayotarajiwa.    

(Chanzo: USAID Learning Lab)

VE Shughuli za Makundi yenye Itikadi Kali Zinazohimiza Matendo ya Vurugu

Shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu ni kauli inayorejelea kutetea, kushiriki, kutayarisha au vinginevyo kuunga mkono matendo ya vurugu yanayochochewa kidhana ili kuendeleza malengo ya kijamii, kiuchumi au kisiasa.""

(Chanzo: Yametolewa kutoka kwenye nyenzo ya The Development Response to Violent Extremism and Insurgency Policy, USAID, 2011)

Miktadha ya Shughuli za VE  

Kuelewa miktadha ya shughuli za VE kunahitaji kufanywa kwa uchanganuzi wa uhusiano kati ya malalamiko ya jamii, vishawishi muhimu, vigezo vinavyosababisha uhamasishaji, misukumo ya nje, viwango vya vurugu na matukio yanayoweza kusababisha shughuli hizi ili kubainisha jinsi ambavyo mashirika ya VEO hutumia mazingira yake ya utendakazi na kushikanisha na miktadha ya mgogoro wa eneo. Ubainishaji wa uwezekano wa kuathiriwa dhidi ya urahisi wa kulengwa na VEO husaidia kutenga hatari na kutambua miundo, mifumo, [weka koma] au watu wa kushiriki katika mazungumzo, kunaweza kuleta athari nzuri kwenye miktadha ya shughuli za VE.

(Chanzo: Yametolewa kutoka kwenye nyenzo ya the U.S. Department of State & USAID's Joint Strategy on Countering Violent Extremism, 2016)

VEO Shirika la Kundi lenye Itikadi Kali Zinazohimiza Matendo ya Vurugu

Kikundi au shirika linalolenga kuendeleza ajenda ya dhana za itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu.

(umetolewa kutoka kwenye nyenzo mbalimbali)