Kwa nini Mafunzo na Marekebisho ni muhimu?

Kama ilivyoshughulikiwa kwenye Moduli ya Kukadiria, unaweza kuanzisha mradi wako kwa kukusanya maelezo (k.m., kupitia ukadiriaji wa shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu au ukadiriaji wa hatari) ili yakusaidie katika kubuni mpango na utekelezaji. Ingawa hatua hii ni muhimu, ni muhimu pia kuendelea kujifunza wakati wote wa utekelezaji wa mradi na kufanya marekebisho panapohitajika ili kuhakikisha kuwa mradi unaendelea kuwa na ufanisi na ufaafu. Hii kweli katika miradi mingi ya maendeleo, lakini ni kweli hasa kwa miradi inayoshughulikia shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu (VE). Marekebisho ni muhimu katika kushughulikia mabadiliko ya shughuli za VE na miktadha ya mgogoro na kiwango chake cha juu cha uchangamano.

Uchangamano wa asili unaopatikana katika miradi ya P/CVE ni wa aina mbili: uchangamano wa tatizo na uchangamano wa kimuktadha.

Uchangamano wa tatizo 

Uchangamano wa tatizo inamaanisha matatizo yanaangazia zaidi muktadha mahususi katika hali ambapo huwezi kutumia suluhu ya muktadha mmoja kwenye mwingine. Inamaanisha pia kuwa matatizo yana vipengele vingi; vipengele vya shughuli vinahusiana kwa njia zisizotabirika, hali ambayo inafanya iwe vigumu kubashiri jinsi shughuli mahususi itakavyoathiri matokeo—na hivyo basi kuhitaji kuendelea kuchunguzwa.

Ni baadhi ya vigezo gani ambavyo vinachangia katika uchangamano wa shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu na kuhitaji miradi ya P/CVE kujumuisha mafunzo na marekebisho?

  • Wahusika wa shughuli za VE huwa wepesi kubadilisha usemi, mikakati, malengo na njia zao utendakazi. Lazima mpango uende sambamba na hali hii, lakini unaweza tu kufanya hivyo ikiwa umebuniwa kwa mbinu sahihi ya ufuatiliaji na uchanganuzi wa miktadha ya shughuli za VE.
  • Matukio ya VE yanapotendeka katika mazingira yaliyoathiriwa na mgogoro, kuna uwezekano wa muktadha kubadilika hasa. Hatua ya kuendelea kufahamu mabadiliko katika muktadha itakuwa kazi muhimu hasa kwa mashirika ya eneo.
  • Kufuatilia jinsi ambavyo vigezo vya kiwango cha kitaifa au kimuundo vinahusiana na kiwango cha eneo, ambapo kuna uwezekano wa miradi mingi kutokea, ni muhimu katika kuelewa jinsi muktadha wa shughuli za VE huenda ukawa unabadilika. 
  • Njia za serikali kuu za kushughulikia hali hiyo zinaweza pia kubadilika kwa haraka na uhusiano kati ya njia hizo za ushughulikiaji na shughuli za VE lazima ufuatiliwe na athari yake kueleweka. 
  • Bado P/CVE ni nyanja mpya na haina msingi thabiti wa ushahidi—hasa data kuhusu shughuli ambazo zimethibitishwa kuwa fanisi katika miktadha mbalimbali.

Yametolewa kwenye : Chanzo

Uchangamano wa kimuktadha 

Uchangamano wa kimuktadha unaweza kuathiri mradi hata kama tatizo lenyewe si changamano. Katika nchi zisizo na usalama thabiti na zilizoathiriwa na mgogoro au katika mazingira ya dharura ya kutoa msaada wa kibinadamu, hata kushughulikia matatizo “rahisi” kunahitaji kufanywa kwa marekebisho.

Title
Mafunzo na Marekebisho Yanawezaje Kushughulikia Mipango ya P/CVE? 

Kujifunza

Kujifunza kunaweza kuchukua aina nyingi na kutumikia malengo tofauti. Kujifunza ni pamoja na mbinu yako na vitendo vinavyohusiana vya kukusanya na kuchambua data inayohusiana na suala ambalo unalenga, shughuli unazotekeleza, na muktadha unaofanyika, ili kuzalisha masomo ambayo unaweza kujirudia. programu yako (kipande cha kujifunza na kukabiliana na hali ya "kukabiliana").

Nyenzo hii Nyenzo hii inaangazia umuhimu wa kujifunza ili kufahamisha kukabiliana na hali katika utayarishaji wa programu. Pia inaelezea aina mbili za mafunzo unazoweza kufanya:

Mafunzo ya Mfuatano

Tambua shughuli moja au zaidi zinazohusiana (kwa mfano, jarida linaloongozwa na vijana linaloangazia masuala yanayohusiana na vijana wanaokabiliana na shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu katika jamii yao) na uweke mazoezi ya mafunzo wakati wa utekelezaji ili kukadiria hatua zinazopigwa na kutambua mafunzo yaliyopatikana. Mafunzo haya bila shaka yatasababisha mabadiliko na marekebisho kwenye mbinu na shughuli. Kwa mfano, mpango wa mafunzo wa jarida linaloongozwa na vijana unaweza kutambua kuwa redio inaweza kufikia zaidi hadhira yake ya vijana, na kwa hivyo mpango unaweza kuamua kuongeza kipengele hicho kwenye mbinu yake.

Mafunzo sambamba

Tekeleza zaidi ya shughuli moja au vikundi vya shughuli zinazohusiana kwa wakati mmoja (kwa mfano, jarida linaloongozwa na vijana lililounganishwa na shughuli tofauti ili kuunda vilabu vya uraia shuleni ili kuhimiza amani na kushiriki katika jamii) na utekeleze shughuli za mafunzo ili kukadiria hatua zinazopigwa na kutambua mafunzo yaliyopatikana. Kwa kutekeleza mbinu mbili kwa wakati mmoja na kuchanganua matokeo ya shughuli zote mbili, unaweza kuelewa mbinu inayofanya kazi vizuri zaidi na kufanya marekebisho yoyote yanayohitajika.

Kidokezo cha Utekelezaji

TUMIA AINA ZOTE MBILI ZA MAFUNZO YA MFUATANO NA MAFUNZO SAMBAMBA

Usichukulie aina hizi mbili za mafunzo kama aina tofauti au zisizoweza kutendeka kwa wakati mmoja – zinaeleza njia za msingi ambazo unaweza kutumia katika kubuni mbinu yako ya mafunzo. Kihalisia, unaweza kutekeleza shughuli za mafunzo ambazo zinatumia aina zote mbili za mafunzo ya mfuatano na mafunzo sambamba kwa wakati mmoja.

MAREKEBISHO

Urekebishaji hurejelea kile unachofanya na data uliyokusanya na mafunzo ambayo umetoa; inarejelea hatua ambazo mradi wako utachukua kwa kujibu yale uliyojifunza. Kulingana na nyenzo ya The Asia Foundation ya Majaribio ya Mkakati: Mbinu Bunifu ya Kufuatilia Mipango ya Misaada Inayobadilika Sana, kwa kawaida sababu tatu husababisha miradi ya maendeleo kurekebishwa. Tumebadilisha sababu hizi ili zitumike kwenye miradi ya P/CVE.

1
Details
Timu hupata au kufikia maelezo mapya

Katika mchakato wote wa utekelezaji wa mradi, timu huendelea kuchanganua maelezo (kuanzia kwa matokeo ya ukadiriaji rasmi wa shughuli za VE hadi kwa maarifa ya wanatimu) hivyo basi kuelewa zaidi na kwa undani muktadha wa eneo na tatizo. Mahusiano yanatokana na kuaminiana mara nyingi huwa muhimu katika kupata maelezo mapya, hasa maelezo kuhusu mada nyeti kama vile shughuli za VE. Washirika na wadau wengine muhimu huenda wasitoe maoni yao ya kweli au maelezo ya ndani hadi watakapoamini mwanatimu kwa kiwango cha kutosha. Hii ndiyo sababu maelezo yanayopatikana katika hatua ya kubuni ya mpango mara nyingi huwa si kamili.

2
Details
Mabadiliko ya nje au kubadilika kwa muktadha

Ingawa ni vigumu kuorodhesha mabadiliko yote ya nje ambayo yanaweza kusababisha timu kufanya marekebisho, mabadiliko kama hayo yanaweza kujumuisha kuanzishwa kwa shirika jipya linaloangazia mradi wa P/CVE, sera mpya ya kimataifa au ya nchini ya kukabiliana na ugaidi, mabadiliko ya serikali, matukio ya kiusalama au kigaidi au mabadiliko mengine ya muktadha ambayo yanaathiri tatizo, wadau au wanufaishwa wa mradi au jamii kwa ujum.

3
Details
Vizuizi na mafanikio

Mpango wako ni dhana ya kimaarifa inayotokana na maelezo uliyo nayo kwa wakati huo kuhusu njia bora ya kutimiza lengo la mradi wako wa P/CVE. Kukumbana na kizuizi, kama vile wanajamii kukataa kushiriki katika mradi unaolenga kuzuia shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu, si kikwazo hasa—kinaweza kukupa maarifa muhimu kuhusiana na jinsi ya kubuni shughuli au kuhitaji kukuza hali ya uaminifu ambayo itazidisha uwezekano wa kupata matokeo bora.

Kulingana na nyenzo hii juu ya usimamizi wa urekebishaji, kuna aina mbili kuu za urekebishaji:

Marekebisho ya Kiufundi

Marekebisho ya kiufundi inarejelea kurekebisha shughuli kulingana na maoni au maelezo ya shughuli ya ufuatiliaji. Aina hii ya marekebisho kwa kawaida hulenga kuboresha utendaji wa mradi na utekelezaji au kuhusu kushirikisha jamii au wanufaishwa kwa njia bora kwenye shughuli zilizopangwa.

Marekebisho ya Kimkakati

Marekebisho ya kimkakati inarejelea marekebisho makubwa ya mwelekeo, kulingana na mafunzo au maoni ambayo yanachunguza ufaafu wa mbinu ya mradi na shughuli zilizopangwa. Kwa mfano, haya yanaweza kuwa mafunzo ambayo yanasababisha mabadiliko katika matokeo ya mradi, kuongeza au kuondoa shughuli au kubadilisha kikundi lengwa.

UDHIBITI UNAOBADILIKA

Udhibiti unaobadilika ni mfumo mpana wa kushughulikia mafunzo na marekebisho katika miradi ya maendeleo. Inahusisha kufuatilia, kujifunza na kukusanya maoni unapotekeleza mradi. Jambo muhimu hata zaidi ni kwamba, inahusisha kufanya marekebisho na mabadiliko ya mwelekeo kutokana na mafunzo yaliyopatikana. Shirika la USAID linafafanua udhibiti unaobadilika kama “mbinu ya kimakusudi ya kufanya maamuzi na marekebisho kutokana na maelezo mapya na mabadiliko ya muktadha.” Kwa hivyo, udhibiti wa marekebisho haihusu kubadilisha malengo wakati wa utekelezaji wa mradi; inahusu kubadilisha mwelekeo unaotumiwa kutimiza malengo husika kutokana na mabadiliko.

PATA MAELEZO HAYA KATIKA MAKTABA YETU YA NYENZO

Baadaye katika moduli hii tutaangalia kwa undani zaidi miundo ya USAID na mashirika mengine kwa kutumia ujifunzaji na urekebishaji na mifumo ya usimamizi inayobadilika.