Utekelezaji wa Mradi

Jinsi ambavyo shirika huanzisha na kutekeleza mradi wa aina yoyote hutegemea nyenzo, uwezo, taratibu zake za ndani, na mara nyingi masharti ya mfadhili ambayo linapaswa kufuata. Hata hivyo, utekelezaji unapaswa kuanza kila wakati na awamu ya kuweka mpango ambapo shirika huratibu nyenzo na miundo inayohitajika ili kuhakikisha kuwa mradi unaanzishwa bila tatizo na utekelezaji fanisi wa shughuli. Mpango huu unajumuisha kukamilisha hati muhimu za mradi, kama vile mpango wa kazi na bajeti au kukamilisha hatua muhimu za utendakazi, kama vile kuandika wafanyakazi wanaohitajika na kuwafungulia ofisi.

VIDOKEZO VYA UTEKELEZAJI

JE , UNGEPENDA KUPATA MAELEZO ZAIDI KUHUSU USIMAMIZI NA UTEKELEZAJI WA MRADI?

Tembelea NGOConnect, mfumo wa mtandaoni unaosimamiwa chini ya mpango wa shirika la FHI 360 wa Uimarishaji wa Asasi za Kiraia Ulimwenguni (FHI 360's Strengthening Civil Society Globally) ili kushiriki nyenzo na maarifa kwa jamii ya kimataifa ya CSO. Mfumo huu una nyenzo kuhusu usimamizi wa mradi, usimamizi wa fedha, uongozi, rasilimali watu, ufuatiliaji na utathmini, maendeleo jumuishi na zaidi.

Hatua za utekelezaji wa miradi ya P/CVE zina masharti yanayofanana na ya utekelezaji wa miradi ya sekta nyingine. Hata hivyo, kulingana na unyeti na muundo wa mpango huu, awamu ya utayarishaji na uanzishaji inaweza kuwa pana zaidi na kuchukua muda mwingi kuliko ya miradi ya aina nyingine. Kwa mfano, mradi wa P/CVE unaweza kuhitaji ukadiriaji wa kina zaidi wa hatari na muda na juhudi nyingi ili kubuni mpango wako wa mawasiliano na uhamasishaji wa wadau, kulingana na unyeti wa shughuli katika baadhi ya jamii.

Unapojitayarisha kutekeleza mradi wako wa P/CVE, zingatia hatua zifuatazo:

  • Tekeleza ukadiriaji wa uwezo (wa shirika, timu na/au washirika wako) ili ubainishe mapengo au mahitaji ya kushughulikia wakati wa utekelezaji. Maelezo zaidi kuhusu ukadiriaji wa kibinafsi wa uwezo wa shirika yamejumuishwa kwenye ukurasa wa Udumishaji.
  • Buni mpango wa kazi ili uweze kuratibu na kupanga shughuli katika hatua zote za mradi. Baada ya kukamilisha kuunda rasimu ya kwanza ya mpango wa kazi, unaweza kuratibu kipindi cha uthibitishaji ili kuonyesha mpango wa kazi na shughuli zinazopendekezwa kwa washirika na/au wanufaishwa ili upate maoni yao.
  • Buni au kamilisha toleo la kwanza la hati za mwongozo wa utekelezaji, ambapo nyingi ya hati hizo zitaanza kutumiwa wakati wa awamu za Kukadiria na Kubuni. Hati hizi zinaweza kujumuisha yafuatayo (angalia Sehemu husika ya Jumla ili upate maelezo ya ziada):
  • Kamilisha mpango wa Ufuatiliaji, Utathmini, na Mafunzo.
  • Kamilisha mpango wa usimamizi wa mradi ili kuhakikisha utaratibu fanisi wa kazi na upatikanaji wa matokeo kulingana na mpango wa kazi.

 

Title
Udhibiti Unaobadilika

Utafiti na uzoefu wa utekelezaji wa mradi wa shirika la FHI 360 unaangazia umuhimu wa kutumia mbinu ya udhibiti unaobadilika badala ya mbinu za usimamizi wa kawaida ambazo hutumiwa na mashirika kwa kawaida. Udhibiti unaobadilika unahusisha ufuatiliaji, mafunzo na kukusanya maoni wakati wa utekelezaji wa mradi. Muhimu zaidi, mbinu hii inajumuisha kufanya marekebisho kulingana na mafunzo haya. Moduli ya Mafunzo inatoa maelezo zaidi kuhusu mifumo ya udhibiti unaobadilika na mafunzo na marekebisho ya miradi ya P/CVE.