Udhibiti wa Hatari

UDHIBITI WA HATARI INAMAANISHA NINI?

Udhibiti wa hatari ni mbinu ya kimfumo na mchakato wa kudhibiti hali zisizotabirika ili kupunguza hasara na madhara yanayoweza kujitokeza na kuboresha fursa na manufaa yanayoweza kupatikana. Lengo la udhibiti wa hatari ni “kuweka utaratibu bora wa hatua za kuchukuliwa chini ya hali zisizotabirika kwa kutambua, kukadiria, kuelewa, kufanya maamuzi na kushughulikia masuala ya hatari.” Udhibiti wa hatari ni mchakato muhimu wa uwezeshaji: kuliko kutoa maamuzi ya kukomesha mpango, michakato fanisi ya udhibiti wa hatari huunda hali zinazohitajika ili mradi uendelee na bila shaka kufaulu. Angalia nyenzo iliyo hapa chini. 

HATARI NI NINI KATIKA MUKTADHA WA MRADI?

Shirika la Shirika la Kimataifa la Usanifishaji (ISO) linafafanua hatari kama “athari ya kutokuwa na uhakika kuhusu malengo.” Athari inaweza kuwa nzuri (ya kuleta manufaa/fursa) au mbaya (ya kutumika tishio, kuchochea uharibifu). Kwa hivyo, hatari inahusisha hali ya kuhitilafiana kwa matarajio. 

KWA NINI MCHAKATO WA UDHIBITI WA HATARI NI MUHIMU KWA MIRADI YA P/CVE?

Kuna hatari katika utekelezaji wa shughuli yoyote ya mradi wa P/CVE. Kwa hivyo, zingatia kutumia mbinu thabiti ya kutambua na kushughulikia hatari katika mchakato wote wa utekelezaji wa mradi. 

PATA MAELEZO HAYA KATIKA MAKTABA YETU YA NYENZO

VIPENGELE VIWILI VYA NYANJA YA P/CVE AMBAVYO VINAFANYA UDHIBITI WA HATARI KUWA MUHIMU

Uwezekano wa kutokea kwa athari mbaya au nzuri ni wa juu hasa.

Ikiwa hatari hazitatambuliwa na kuwekewa mpango katika mradi wa P/CVE, uwezekano wa kutokea kwa madhara kwa watu, jamii na mashirika unaweza kuongezeka zaidi. Kwa upande mwingine, ikiwa tutatambua na kudhibiti hatari ili kusaidia mradi kuboresha utoaji kipaumbele kwa shughuli, ufaafu na ufanisi, watu na jamii zinazohusika katika mradi wa P/CVE wanaweza kuwa uwezo zadi wa kupinga VE katika jamii zao.

Kuna uwezekano wa kiwango cha juu wa kutokea kwa hatari unaposhughulikia mradi wa P/CVE.

Unapofanya kazi katika maeneo yaliyoathiriwa na mgogoro au katika maeneo yaliyo katika hatari ya kuathiriwa na shughuli za VE, unashughulikia masuala ambayo mara nyingi hueleweka vibaya, yana utata na husababisha upinzani. Hali hii huongeza hatari zinazohusiana na sifa za shirika na usalama wa wafanyakazi. Pia, kwa sababu suala la P/CVE ni nyanja mpya kiasi, kuna mijadala inayoendelea na utata kuhusu fafanuzi kuu, vigezo vinavyosababisha shughuli za VE, na kinachofanya kazi au kisichofanya kazi kuhusiana na kuweka mpango wa mradi wa P/CVE.

Kwa kutambua na kudhibiti hatari katika mradi wa P/CVE, unapunguza uwezekano wa kutokea kwa athari mbaya na kuimarisha uwezo wa utekelezaji fanisi na kupatikana kwa athari nzuri ya mradi wako, huku ukilinda jamii, wanufaishwa wa mradi, timu na shirika lako.

Ingawa mbinu za udhibiti wa hatari zinatofautiana kutoka kwa mradi au shirika moja hadi jingine, mbinu hizo kwa kawaida zinajumuisha hatua zilizobainishwa katika jedwali lililo hapa chini.

HATUA YA 1
Tambua hatari

Kwa kawaida unatambua "aina za hatari" ili kuhakikisha kwamba unazingatia awamu au sehemu tofauti za mradi. Aina hizi zinaweza kujumuisha: hatari za kiutendakazi; hatari za kimuktadha; hatari za kiusalama; hatari za kishirika; na hatari za kimpango.

HATUA YA 2
Kadiria hatari

Kwa kila hatari iliyotambuliwa, jibu maswali mawili muhimu:

  • Kuna uwezekano upi wa kutokea kwa hatari hii?
  • Hatari hii itakuwa na athari gani kwa mradi wako?

Kwa kutumia ukadiriaji huu, timu yako inaweza kuorodhesha au kukadiria kwa nambari (kiwango cha chini, kiwango cha wastani, kiwango cha juu) uwezekano na athari inayotarajiwa ya hatari husika. Matokeo ya ukadiriaji huu mara nyingi huonyeshwa katika muundo wa ukadiraiji wa hatari, ambapo kipengele cha uwezekano na athari huwekwa katika jira tofauti, ili kuonyesha hatari ambazo ni muhimu zaidi kuzingatia.

HATUA YA 3
Weka mpango wa ushughulikiaji

Buni mpango wa jinsi ya kushughulikia hatari hizi. Mara nyingi, hatari haziwezi kuondolewa kabisa na mbinu ya kushughulikia hatari hizi inapaswa kubainisha jinsi ya kudhibiti hatari hizi. Mbinu za ushughulikiaji zinazoweza kutumika kwa kawaida huhusisha njia zifuatazo:

  1. Kushughulikia hatari kwa kuchukua hatua za kupunguza uwezekano wa kutokea hatari au athari yake katika mradi wako
  2. Kuhamishia hatari husika kwa shirika au mtu mwingine, kama vile mtoa huduma za bima
  3. Kustahimili hatari kwa kuamua kwamba hakuna uwezekano wa kutokea kwa hatari hiyo au ina athari ya kiwango cha chini zaidi na si muhimu kuzingatiwa
  4. Kuepuka hatari kwa kutotekeleza shughuli inayoweza kusababisha hatari husika

Jedwali hili limeundwa kwa kutumia maelezo ya muhtasari wa udhibiti wa hatari uliotolewa katika nyenzo ya Mwongozo wa Utendakazi kuhusu utayarishaji na utekelezaji wa shughuli zinazofadhiliwa na Umoja wa Mataifa zinazohusiana na kukabiliana na ugaidi na shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu katika nchi zinazokua kiuchumi.

Kuna zana na mifumo kadhaa ya udhibiti wa hatari ambayo unaweza kutumia katika mradi wako. Mfumo wa UNDP wa Udhibiti wa Hatari wa Mipango ya Kuzuia Shughuli za Makundi yenye Itikadi Kali Zinazohimiza Matendo ya Vurugu (PVE): Dokezo la Mwongozo kwa Watekelezaji linaelezea hatua tano muhimu (angalia grafu iliyo hapa chini) za kutumia mchakato wa udhibiti wa hatari katika mradi wako wa P/CVE. Bofya hati hii ya mwongozo mfupi inayotoa muhtasari wa hatua tano za mchakato wa UNDP wa udhibiti wa hatari.

 

riskmanagement

Tazama mfano huu wa Rejista ya Hatari iliyochukuliwa kutoka kwa mwongozo wa UNDP. Rejesta hii ya hatari itakusaidia kukuza mpango wako wa kukabiliana na hatari zilizotambuliwa. 

Title
doc
Additional Resources
photo
Details

Usimamizi wa Hatari za Usalama: Mwongozo wa Msingi kwa NGOs Ndogo

Je, ungependa kujifunza zaidi kuhusu udhibiti wa hatari za usalama? Mwongozo huu unaonyesha mfumo msingi wa usimamizi wa hatari kwa usalama ambao unaweza kusaidia NGOs ndogo kukuza michakato na hatua muhimu ambazo zitaimarisha usalama wa wafanyikazi wao na kuboresha sifa na uaminifu wa shirika lao. Mwongozo huu unajumuisha mwongozo, nyenzo za ziada na violezo vinavyoweza kubadilishwa na shirika lako. 

photo
Details

Mazingatio ya Kutumia Data kwa Uwajibikaji katika USAID

Je, ungependa kujifunza kuhusu hatari zinazohusiana na data na jinsi ya kudhibiti data inayokusanywa na kuzalisha mradi wako? Nyenzo hii inatanguliza mfumo wa kutambua na kuelewa hatari zinazohusiana na data ya maendeleo. Nyenzo hii inaangazia masuala muhimu na inatoa ushauri unaoweza kutekelezeka ili kuwasaidia wale wanaotumia data kuboresha matumizi huku pia wakidhibiti hatari.  

UDHIBITI WA HATARI AU UZINGATIAJI WA MGOGORO: NI MCHAKATO UPI NINAOPASWA KUTEKELEZA?

Jibu rahisi ni: yote miwili! Udhibiti wa hatari na uzingatiaji wa mgogoro mara nyingi huenda pamoja, na baadhi ya mifumo inaweza kuchanganya yote miwili. Kwa mfano, mfumo wa UNDP wa Udhibiti wa Hatari uliotajwa hapo juu unajumuisha mchakato wa uzingatiaji wa mgogoro kama kanuni moja muhimu. Mchakato wa uzingatiaji wa mgogoro unahitajika kwa ajili ya udhibiti fanisi wa hatari kwa sababu kusababisha madhara bila kukusudia kunaweza kuzidisha zaidi hatari kwa shirika, mpango au wafanyakazi.

Shirika la CDA limebundi kikundi cha maswali ambayo yanaweza kukusadia kujumuisha kanuni ya Usisababishe Madhara kwenye uchanganuzi wako wa hatari na mpango wa ushughulikiaji wa hatari.

HATARI ZA MRADI WA P/CVE NI ZIPI?

Hatari zitatofautiana kwa kila mradi kulingana na muktadha na shirika linalotekeleza mradi husika. Mashirika yanaweza kutambua makundi na/au aina za hatari ambazo zitatoa mwongozo wa kubuni mchakato wa udhibiti wa hatari. Mfumo wa UNDP wa Udhibiti wa Hatari unatambua aina tatu za hatari na fursa - hatari za kimuktadha, kishirika na kimpango.

contextual interaction  

Tume ya Ulaya ilibainisha aina au makundi yafuatayo ya hatari: Hatari za Kifedha, Kiutendakazi, Kiusalama, Kisheria, Kisiasa, Kisifa, na Kiusimamizi.

Orodha hii ya mfano inaonyesha hatari ambazo watekelezaji au miradi mingine ya P/CVE imebainisha. Orodha hii si kamilifu, lakini inaweza kusaidia shirika lako kuzingatia makundi na aina za hatari ambazo huenda zinahusiana na mradi wako.