Kabla ya kuanza mradi wako, zingatia maswali yafuatayo:

1
Details
DHANA ZA ITIKADI ZINAZOHIMIZA MATENDO YA VURUGU INAMAANISHA NINI KATIKA MUKTADHA WANGU?

Sehemu hii itaelezea changamoto maalum zilizopo katika ufafanuzi wa dhana ya VE na kuangazia umuhimu wa kuchanganua dhana ya VE katika muktadha wa eneo lako. 

2
Details
HATARI ZAKE NI ZIPI NA TUNAWEZAJE KUTUMIA KANUNI YA UZINGATIAJI WA MGOGORO?

Sehemu hii itafafanua neno “uzingatiaji wa mgogoro” na umuhimu wa kutumia kanuni ya uzingatiaji wa mgogoro katika hatua zote za mradi wa P/CVE.

Title
3

JE, TUNALENGA KUZUIA AU KUKABILIANA NA SHUGHULI ZA MAKUNDI YENYE ITIKADI KALI ZINAZOHIMIZA MATENDO YA VURUGU?

Shirika la USAID na US Department of State yanafafanua miradi ya kuzuia au kukabiliana na shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu (P/CVE) kama: “hatua za mapema za kukabiliana na shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu za kushawishi, kuandikisha na kuchochea wafuasi wake kutekeleza matendo ya vurugu na kushughulikia vigezo mahususi ambavyo vinafanya watu kushawishika na kujiunga na makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu ili kutekeleza matendo ya vurugu. Hii inajumuisha kukatiza mbinu zinazotumiwa na makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu kuvutia watu kujiunga kwenye matendo ya vurugu na kubuni njia, nadharia, uwezo na mbinu mbadala za kudumisha hali ya kutoshawishika katika jamii na watu wanaolengwa ili kupunguza hatari ya kushawishika na dhana za itikadi kali na watu kujiunga kwenye matendo ya vurugu.”  

PATA MAELEZO HAYA KATIKA MAKTABA YETU YA NYENZO  
Kuzuia Shughuli za Makundi Yenye Itikadi Kali Zinazohimiza Matendo ya Vurugu (PVE) dhidi ya Kukabiliana na Shughuli za Makundi Yenye Itikadi Kali Zinazohimiza Matendo ya Vurugu (CVE)

Tofauti kati ya miradi ya CVE na PVE inaweza kuonyesha jinsi ambavyo wafadhili au wataalamu wa maendeleo huainisha kazi yao. Ingawa maneno CVE na PVE hutumika kwa kubadilishana, mbinu hizi ni tofauti kiasi, hasa unapoondoka kwenye suala la nadharia hadi kwenye utekelezaji halisi. Picha iliyo hapa chini, inayoonyesha mpangilio maalum wa mradi wa P/CVE kulingana na mbinu tofauti za ushughulikiaji, inatoa njia muhimu ya kuwazia kuhusu jinsi mbinu hizi zinavyoweza kutofautiana. Aina ya watu unaolenga kushirikisha kwenye mradi wako bila shaka wataathiri muundo wa mpango wako. Mbinu, matokeo na hatari zinazohusiana na mbinu hizi tofauti za ushughulikiaji zitatofautiana zaidi.

 

Kuna pia tofauti muhimu kati ya kukabiliana na ugaidi (CT) na kukabiliana na shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu (CVE). Angalia picha iliyo hapo chini.

 

KUKABILIANA NA UGAIDI (CT)

Shughuli zinazolenga kudhibiti, kukomesha na kufuatilia magaidi na shughuli za kigaidi.

 

Dhidi ya

Dhidi ya

KUKABILIANA NA SHUGHULI ZA MAKUNDI YENYE ITIKADI KALI ZINAZOHIMIZA MATENDO YA VURUGU (CVE)

Shughuli za kutohalalisha na kuzuia watu kujiunga na makundi ya kigaidi yaliyopo na kushughulikia vigezo vinavyowezesha shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu kunawiri na kuungwa mkono.

Uko tayari? Tuanze!