Kuchagua Shughuli Zako

Ukadiriaji wako wa shughuli za VE na Nadharia yako ya Mabadiliko vitasaidia katika uteuzi wa shughuli zako. Jedwali lililo hapa chini linatoa baadhi ya mifano ya sehemu za kushughulikia za visababishi vya shughuli za VE vilivyobainishwa. Hiki ni chanzo cha jinsi ya kuhusisha shughuli zako na vigezo vya msukumo na mvuto ulivyobainisha kupitia ukadiriaji wa visababishi vya shughuli za VE.

Kigezo Visababishi vya Shughuli za VE Mifano ya Shughuli za Mradi wa P/CVE
Mazingira Yanayochangia
  • Nchi Zisizo Thabiti 
  • Usalama duni na/au ufisadi
  • Maeneo yenye uongozi duni au uongozi mbaya 
  • Ajenda ibukizi za kidini 
  • Migawanyiko ya kidini ya ndani na nje 
  • Ufadhili wa serikali wa makundi ya vurugu 
  • Mafunzo ya vyombo vya kulinda usalama au wawakilishi wa serikali 
  • Mazungumzo ya kidini ya ndani na/au nje
Msukumo
  • Visababishi vya Uchumi wa Kijamii: kutengwa na kutojumuishwa kijamii, ubaguzi wa kijamii, kushindwa kutimiza matarajio na ukosefu wa rasilimali muhimu za kuboresha maisha katika jamii
  • Visababishi vya Kisiasa: kunyimwa haki za kisiasa na uhuru wa kiraia, kukandamizwa na serikali na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, uhusiano na nchi za nje, uvamizi wa kisiasa na/au kijeshi, ufisadi uliokithiri na kutoadhibiwa kwa watu wenye mali na hadhi ya juu katika jamii, mgogoro wa eneo, serikali zisizotambuliwa na ukosefu au udhibiti wa upinzani unaotambuliwa kisheria, kutishwa au kushawishiwa na VEO, dhana kwamba mfumo wa kimataifa kimsingi hautendi haki na una uhasama na kabila na imani yao ya kidini
  • Visababishi vya Kitamaduni: hisia kwamba dini au kabila la mtu fulani limevamiwa au vitisho pana vya kitamaduni vinavyotishia tamaduni, mila, maadili na hisia ya vitisho vya jumla kwa hadhi na heshima ya mtu binafsi
  • Mipango ya ushirikishaji na uwezeshaji wa vijana
  • Fursa za kiuchumi kwa vijana
  • Elimu
  • Kushirikisha wanawake katika miradi ya P/CVE
  • Kuboresha uongozi/kushughulikia malalamiko yanayohusiana na suala la uongozi
  • Kushirikisha wawakilishi wa kidini katika miradi ya CVE
  • Kampeni za utetezi na uhamasishaji wa haki za binadamu
  • Kuimarisha uthabiti na maendeleo ya jamii
  • Ushirikishaji wa wadau katika jamii
  • Kubuni sera zinazolenga jamii
Mvuto
  • Hisia ya kukubaliwa
  • Uhalalishaji na kuruhusiwa kwa tabia za asili za vurugu
  • Kuwepo kwa makundi ya VE yenye nadharia zenye ushawishi na malengo ya kuvutia
  • Kuwepo kwa maeneo au mifumo yenye itikadi kali
  • Mitandao ya kijamii na miktadha ya kikundi
  • Utoaji wa huduma (kushughulikia mahitaji na matarajio yaliyoshindwa kutimizwa)
  • Zawadi halisi, tamaa au kuenezwa kwa shughuli haramu za kiuchumi
  • Kushirikisha wanafamilia na washawishi wengine
  • Usaidizi wa kisaikolojia na kijamii na udhibiti wa kiwewe  
  • Ujumbe au nadharia pinzani au mbadala
  • Kutenga watu na dhana za itikadi kali  
  • Njia mbadala za kushughulikia watu wenye dhana za itikadi kali/FTF badala ya kufungwa gerezani  
  • Urekebishaji wa tabia za FTF  
  • Kujumuisha tena FTF katika jamii
  • Shughuli zinazolenga mtu binafsi

 

Unapochagua shughuli zako, zingatia: 

SHIRIKA LAKO LINA UWEZO GANI WA KUTEKELEZA SHUGHULI AMBAZO UMECHAGUA?  

Je, kwa sasa unafanya kazi katika eneo au sehemu fulani yenye changamoto? Ikiwa ni hivyo, unaweza kupanua au kubadilisha shughuli zako ili kushughulikia vigezo au makundi ambayo umebainisha? Ikiwa sivyo, unaweza kupanua maeneo ya mradi wako? Ni nini kitakachohitajika ili kufanya hivyo? Uwezo na mapungufu ya shirika lako vinaweza kubainisha sehemu za miradi ambazo unaweza kushughulikia kwa ufanisi. 

UNAWEZAJE KUSHIRIKISHA WAHUSIKA WENGINE KWA NJIA BORA ILI KUPANUA ATHARI ZA MRADI WAKO? 

Zingatia wadau muhimu unaopaswa kushirikisha na jinsi ya kukuza ushirikiano wa kimkakati kwa njia bora na watu, mashirika na mitandao mingine ili kubuni mbinu pana au kikundi cha shughuli.    

UTAHAKIKISHAJE KUWA SHUGHULI ZAKO HAZISABABISHI MADHARA?  

Rejelea Sehemu ya Jumla kuhusu Uzingatiaji wa Mgogoro ili uone maswali unayopaswa kuuliza na majedwali ya kazi unayopaswa kutumia, kuhusu jinsi ya kubuni shughuli zako kwa njia bora ili zisizidishe vitenganishi katika jamii bila kukusudia na ili pia ziimarishe viunganishi.

Title
doc
ZOEZI LA KUBUNIA SHUGHULI
photo
Details

Karatasi ya Usanifu wa Shughuli

Karatasi hii itakusaidia kuunda mradi wako.

Title
Kuhakikisha kwamba Mradi Wako Hausababishi Madhara

Baada ya kukamilisha uchanganuzi wako wa vitenganishi na visababishi, unaweza kutumia mfumo ulio hapa chini ili ukusaidie kuhusisha uchanganuzi wako na muundo na mpango wa shughuli za mradi wako.

Baada ya kuvipa kipaumbele vitenganishi na viunganishi (angalia zoezi lililo hapa chini), unaweza kuzingatia chaguo na fursa.

  • Vitenganishi na viunganishi hivi vinawezaje kubadilishwa? Yaani, ni dhana gani ambazo zinaweza kupunguza/kuzuia vitenganishi hivyo na ni dhana gani ambazo zinaweza kuongeza/kukuza viunganishi hivyo?
  • Timu yako inaweza kufanya nini ili kuleta mabadiliko mazuri? Ni nini unachofanya ambacho kinaathiri au kinaweza kuleta athari mbaya? Kwa nini athari hiyo mbaya imetokea? Ni nini ambacho unaweza kubadilisha ili kushughulikia athari hiyo? Hatua ya kuelewa vitendo na tabia itasaidia katika kubuni mkakati wako wa utekelezaji (imefafanuliwa zaidi kwenye Moduli ya Kutekeleza).
  • Ni fursa na chaguo gani zinazohusishwa na viashirio ulivyobuni katika Hatua ya 2 wakati wa ukadiriaji wa Visababishi na Viunganishi kwenye Moduli ya Kukadiria?
  • Utafuatiliaje mabadiliko yaliyosababishwa na mradi wako? Hatua hii itasaidia katika kubuni mkakati wako wa ufuatiliaji na utathmini (imefafanuliwa zaidi kwenye Moduli ya Kufuatilia na Kutathmini).
  • Ikiwa hakuna mabadiliko yatakayotokea, una chaguo lingine? Je, umebuni mchakato wa kufahamu ni kwa nini mabadiliko hayajaleta athari unayotarajia? Hatua hii itasaidia katika kubuni mpango wako wa mafunzo (imefafanuliwa zaidi kwenye Moduli ya Mafunzo).
Title
doc
ZOEZI LA UTANGULIZI WA VIGAWANAJI NA VIUNGANISHI
photo
Details

Karatasi ya Kazi ya Kuweka Kipaumbele kwa Vigawanyiko na Viunganishi

Karatasi hii itakuongoza katika zoezi hili.