Njia za Uthibitishaji/Ukusanyaji wa Data

logframe2

Njia za Uthibitishaji ni zana ambazo hutumika na michakato inayofuatwa ili kukusanya data inayohitajika ili kukadiria hatua zilizopigwa. Data inayokusanywa inaweza kuwa takwimu za data au data ya uchanganuzi. Data ya uchanguzi ni wazi zaidi na mara nyingi hukusanywa kupitia mahojiano, makundi lengwa na njia nyingine za ukusanyaji wa data ya uchanganuzi. Data ya takwimu hutumika kujibu maswali kama vile, ngapi, mara ngapi, kiwango gani na kiasi gani, na mara nyingi hukusanywa kupitia tafiti.

Njia za ukusanyaji wa data zinaweza kuwa na muundo kamili, muundo usio kamili au zisizo na muundo wowote.

MANUFAA NA MAPUNGUFU YA NJIA KUU ZA UKUSANYAJI WA DATA KATIKA MUKTADHA WA MRADI WA P/CVE:

  Manufaa katika muktadha wa mradi wa PVE   Mapungufu katika muktadha wa mradi wa PVE
Tafiti Njia ya kukusanya maelezo na maarifa kuhusu mada husika, mara nyingi kupitia karatasi au hojaji za mtandaoni.
  • Hali ya kutotambuliwa inaweza kusababisha kutolewa kwa majibu ya kweli zaidi
  • Zinaweza kukusanya maelezo kutoka kwa watu wengi
  • Ni za gharama ya chini
  • Majibu hupatikana haraka
  • Wahojiwa wana muda wa kuzingatia majibu yao
  • Hufanywa na watu wanaoweza kutumia intaneti/simu pekee
  • Mshiriki hawezi kuuliza iwapo haelewi swali
  • Kasi za kujibu zinaweza kuwa za kiwango cha chini
  • Haziulizi maswali ya ufuatiliaji
Mazungumzo ya Kikundi Lengwa Kikundi cha washiriki, kwa kawaida wenye sifa zinazofanana (umri, jinsia, kazi, n.k), huulizwa mitazamo yao kuhusu mradi au mada mahususi. Mazungumzo ya makundi lengwa huelekezwa kwa makini na mtu mwingine na kwa kawaida hujumuisha washiriki 6 hadi 10.
  • Hulenga mada mahususi kama vile tatizo la jamii
  • Mazungumzo husababisha kutolewa kwa maoni ya aina nyingi
  • Hutoa fursa ya kubadilishana mawazo na wengine ambao huenda wana mtazamo tofauti (k.m. viongozi wa vijana wanaweza kujifunza kutoka kwa maofisa wa polisi na vile vile maofisa wa polisi wanaweza kujifunza kutoka kwa viongozi wa vijana)
  • Huruhusu maelezo kuthibitishwa papo hapo
  • Mapendeleo ya msimamizi: Msimamizi anaweza kudokeza kuhusu au kubainisha mapendeleo yake ya kibinafsi, hali ambayo husababisha ukinzani wa matokeo
  • Mapendeleo ya kijamii: washiriki wanaweza kujibu maswali kwa njia isiyo ya haki ili wapendelewe na washiriki wengine (k.m. vijana wanaweza kujibu kwa njia tofauti ikiwa polisi wako chumbani nao)
  • Makubaliano ya kikundi: washiriki wanaweza kukubaliana na wengine katika kikundi ili kupunguza tu kiwango cha mgogoro, ingawa kihalisia wana maoni tofauti
  • Ukosefu wa hali ya kutotambulishwa: huenda washiriki wasitoe maelezo nyeti (k.m. huenda kijana asiwe huru kutoa maelezo kuhusu uhusiano wake na kikundi cha shughuli za VE)
Mahojiano ya Watoa Habari Muhimu Mahojiano ya ana kwa ana; yanaweza kuwa na muundo kamili, yasiwe na muundo kamili au yasiwe na muundo wowote. Wahojiwa wanaweza kuwa maofisa wa serikali, wafanyakazi wa NGO, wawakilishi wa sekta ya kibinafsi, viongozi wa kidini, wasomi, n.k. 
  • Hukusanya maelezo ya kina kuhusu mada mahususi kutoka kwa mtaalamu
  • Huruhusu uchunguzi wa kina wa dhana ambazo huibuka kutoka kwenye mbinu nyingine
  • Matokeo yanaweza kuwa na mapendeleo: huhitaji mahojiano yafanywe kwa idadi kubwa ya wahojiwa wenye mitazamo tofauti
  • Inaweza kuwa vigumu kutambua “wataalamu”
  • Inaweza kuwa vigumu kuratibu
  • Huchukua muda mwingi
Uchunguzi Aina mbili za uchunguzi: 1) Uchunguzi unaofanywa na mtu asiyeshiriki ni mbinu ambapo mchunguzi hana uhusiano wa moja kwa moja na mradi. 2) Uchunguzi unaofanywa na mshiriki hufanyika wakati ambapo mchunguzi anashirikiana moja kwa moja na watu anaochunguza (k.m. kujiunga na kikundi cha watu au shirika) na kushiriki katika shughuli ambazo zinachunguzwa.
  • Inaweza kutumiwa kubainisha ni kwa nini mradi haufanyi kazi vizuri
  • Inaweza kutumiwa wakati ambapo ni vigumu kutumia mbinu rasmi za ukusanyaji wa data, kama vile wakati kikundi fulani cha watu hakipendelei kuhojiwa.
  • Inaweza kuchunguza matukio ambayo yanasababisha shughuli za VE, kama vile hotuba ambazo zinahimiza matendo ya vurugu.
  • Inaweza kuwa vigumu kufikia makundi
  • Inaweza kuwa hatari katika miktadha fulani ya shughuli za VE
  • Huchukua muda mwingi kupata data ya kutosha
  • Inatumika katika idadi ndogo ya mazingira
  • Kwa uchunguzi unaofanywa na mshiriki, washiriki wanaweza kuchukua muda kuamini mchunguzi

* Maelezo yaliyo kwenye jedwali lililo hapo juu yametolewa kwenye: Nyenzo ya shirika la International Alert/UNDP ya Kukabili Misimamo Mikali ya Vurugu na Kupunguza Hatari: Mwongozo wa Usanifu na Tathmini ya Mpango (angalia ukurasa wa 110 ili upate maelezo zaidi kuhusu aina mahususi za tafiti na mbinu shirikishi za ukusanyaji wa data); ATHARI Ulaya: Zana ya Tathmini kwa wataalamu wanaofanya kazi katika uwanja wa kukabiliana na itikadi kali; na “Kubuni kwa ajili ya Matokeo: Kuunganisha Ufuatiliaji na Tathmini katika Mipango ya Mabadiliko ya Migogoro” (ukurasa wa 207 hadi 209) ili uone manufaa na mapungufu ya njia za ziada za ukusanyaji wa data.