Hatari na Dhana

Hatari na dhana ni vigezo vya nje ambavyo mradi hauna uwezo wa kuvidhibiti, lakini vinaweza kuathiri shughuli na matokeo ya mradi. Mara nyingi vigezo huhusishwa na matukio, miktadha na/au dhana za jamii. Hatua ya kutambua hatari na vigezo husaidia shirika kujitayarisha kwa changamoto zinazoweza kujitokeza katika kutimiza malengo ya mpango pamoja na kubainisha iwapo hatua ya kubuni upya mradi inaweza kuwa ya manufaa. Kwa mfano, ikiwa dhana inaonyesha kuwa huenda jamii isikubali shughuli husika, inaweza kuwa muhimu kubuni upya mpango au kuongeza kwanza shughuli za ziada ambazo zitafanya jamii ikubali mpango.

logframe3