Uchunguzi kifani

Title
Ukuzaji wa Uwezo na Kukadiria Athari ya Mawasiliano ya Mabadiliko ya Tabia ya Mradi wa P/CVE

Association Chifae (Chifae) ni shirika la eneo la asasi za kiraia linalopatikana katika jiji la Tangier, Moroko. Shirika la Chifae lilitekeleza shughuli inayofadhiliwa ya miezi saba iliyolenga kuhamasisha vijana wa eneo kuhusu shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu. Mradi huo ulitoa mafunzo kwa wafanyakazi 15 wa umma na wa sekta ya elimu kuhusu mbinu za mawasiliano ili waweze kutekeleza kampeni ya uhamasishaji ya wiki mbili kuhusu masuala ya spoti ili kukuza hali ya ustahimilivu na mshikamano wa kijamii katika eneo la Beni Makkada, jijini Tangier.

Baada ya warsha ya siku tano, wafanyakazi wanne hadi watano wa shirika Chifae (kwa usaidizi wa kiufundi kutoka shirika la FHI 360) walibuni nyenzo za kampeni ya uhamasisha ya shirika la Chifae. Nyenzo hii ilijumuisha mpango wa Ufuatiliaji na Utathmini (M&E) ili kubainisha iwapo kampeni ilikuwa na athari yoyote kwa maarifa, mitazamo na tabia za vijana. Shirika la Chifae lilipanga kupanua kampeni ya mpango ili kujumuisha jiji lote la Tangier. Kwa hiyo, utathmini wa matokeo ya kampeni ya jaribio katika eneo la Beni Makkada ulikuwa muhimu katika kukusanya ushahidi wa kuchangia katika ubunifu wa mipango ya baadaye ya shirika la Chifae.

Shirika la Chifae lilizindua rasmi kampeni yake ya uhamasishaji katika eneo la Beni Makkada mnamo tarehe 18 Juni 2019. Wito wa kampeni ulikuwa #ASpaceforAll, unaorejelea jamii inayoheshimu utofauti wa watu.

Kampeni ilijumuisha vipengele vifuatavyo:

  • Ukurasa wa tukio la Facebook uliosimamiwa na kudhibitiwa na mfanyakazi wa shirika la Chifae. Shirika la Chifae lilitegemea machapisho kadhaa ya picha ambayo yalisambazwa kupitia ukurasa wa Facebook.
  • Tangazo la ukurasa wa tukio kwenye tovuti maarufu ya eneo na kwenye gazeti la kila wiki la eneo (gazeti pekee linalopatikana katika jiji la Tangier).
  • Uonyeshaji wa kauli ya hashitegi na wito wa kampeni kwenye viwanja 15 vya soka vya eneo katika eneo la Beni Makkada.
  • Usambazaji wa fulana 400 za mazoezi ya soka zilizoandikwa wito wa kampeni kwa CSO za spoti za eneo katika eneo la Beni Makkada.
  • Kuweka mabango ya matangazo katika maeneo manne tofauti katika uwanja wa soka jijini Tangier na katika eneo la Beni Makkada.
  • Nafasi ya tangazo la sekunde 30 katika redio ya eneo ambalo lilitangazwa mara nne kwa siku katika kipindi cha wiki mbili kwenye kituo cha redio cha eneo.

Mbinu ya Ufuatiliaji na Utathmini (M&E) na dhana

Shirika la Chifae lilibuni utafiti (uliotafsiriwa katika lugha ya Kidarija cha Moroko) ili kukusanya data ya msingi na ya hitimisho kuhusu dhana, mitazamo na tabia za vijana katika jamii zao. Shirika la Chifae lililenga kuelewa jinsi vijana walivyochukulia suala la ustahimilivu na maadili mengine bora.

Shirika la Chifae lilikusudia kufanya utafiti uwe rahisi ili watu wa kujitolea waweze kukusanya data kwa urahisi kupitia mahojiano ya ana kwa ana. Shirika la Chifae mwanzoni lilipanga kuhoji wahojiwa sawa kuanzia mwanzo hadi mwisho ili kukadiria vizuri athari ya mradi iliyotarajiwa. Mchakato huu ungesaidia shirika la Chifae kuelewa jinsi wahojiwa wanaweza kubadilisha mitazamo au tabia zao kuanzia kabla ya kampeni kuanza hadi baada ya kukamilika. Kwa bahati mbaya, watu wa kujitolea hawakuweza kuhoji wahojiwa sawa baada ya kampeni kukamilika, kwa hivyo ukusanyaji wa data ulijumuisha tu vijana walioshuhudia kampeni ya shirika la Chifae.

Sampuli ya watu waliohojiwa walikuwa vijana 100, ikijumuisha mashabiki vijana wa soka/spoti (na usawa usio kamili wa kijinsia licha ya kanuni za kitamaduni za eneo na vikwazo kuhusu utangamano wa watu wa jinsia tofauti katika maeneo ya umma). Shirika la Chifae lilipanga kila mmoja wa watu sita wa kujitolea akusanye idadi ya juu zaidi ya majibu 20 ya hojaji kwa jumla ya zaidi ya tafiti 100.

Mojawapo ya dhana kuu ilikuwa kwamba wahojiwa wote vijana walikuwa wameona (au kusikia) kampeni ya shirika la Chifae. Swali la kwanza la uchunguzi lilijumuishwa kwenye mchakato. Shirika la Chifae liliamua kulenga viwanja vya soka pamoja na mitaa na viwanja vya soka vya jamii kabla ya kuanza kwa kampeni na kisha tena baada ya kukamilika kwa kampeni.

Shirika la Chifae lilishirikisha vijana wa kujitolea kutoka katika jamii kwa sababu ya ufahamu wao wa muktadha wa eneo na kuwafunza jinsi ya kutekeleza utafiti. Mafunzo yalijumuisha wasilisho kuhusu mradi, kusudi la utafiti na mbinu, pamoja na kanuni za uzingatiaji wa maadili na Usisababishe Madhara.

Title
Muhtasari wa matokeo
Maarifa Mitazamo Tabia
  • 552% ya wahojiwa vijana walifikiria kuwa ujumbe wa kampeni (wito wa kuwa na amani na ustahimilivu ili kushughulikia matukio ya vurugu katika viwanja vya soka) ulitolewa kwa njia dhahiri.
  • Karibu thuluthi mbili (63%) ya wahojiwa wote walikubaliana na ujumbe wa kampeni, wakionyesha imani thabiti katika ujumbe wa jumla kuhusu kustahimili wengine.
  • Karibu nusu (47%) ya wahojiwa wote vijana walisema kuwa walichukulia mashabiki wa timu zingine kwa njia nzuri zaidi mwishoni mwa kampeni.
  • Karibu 30% zaidi ya vijana (kutoka 44% hadi 72%) walijihisi huru zaidi kutangamana na vijana kutoka katika jamii zingine mwishoni mwa kampeni.
  • 34% zaidi ya wahojiwa vijana walisema kuwa hawana utofauti mkubwa na mashabiki vijana wa timu zingine baada ya kushiriki katika kampeni ya #Fada2_Liljami3.
  • Kabla ya kampeni kuanza, thuluthi moja ya vijana walijibu kuwa watakuza uaminifu kupitia uungwana huku 14% pekee wakitaja juhudi za mawasiliano na uhamasishaji kama njia yao ya msingi ya kukuza uaminifu.
  • Mwishoni mwa kampeni, vijana wengi walitaja mawasiliano na mazungumzo (36%) kama njia ya kukuza uaminifu, karibu na idadi sawa ya waliotaja uungwana (39%).

MAFUNZO YALIYOPATIKANA KUPITIA MCHAKATO WA UFUATILIAJI NA UTATHMINI (M&E) WA SHIRIKA LA CHIFAE:

Shirika la Chifae liliweza kuthibitisha kuwa vijana katika eneo la Beni Makkada walikuwa na imani thabiti kwa ujumbe wa jumla wa kustahimili wengine, hali ilioonyesha mfano wa mabadiliko mazuri katika mitazamo kati ya vijana walioshuhudia kampeni ya shirika la Chifae na kuonyesha kuwa kuna uwezekanao zaidi wa vijana kuthamini mawasiliano na vijana wengine kama watu binafsi nje ya mfumo wa mashindano ya spoti. Mafunzo haya yalisaidia shirika la Chifae kupanga kupanua kampeni ili kufikia eneo kubwa na kuiga kampeni ili kutoa uhamasisho kuhusu mada zingine.

Shirika la Chifae lilikadiria athari ya kampeni na kujaribu uwezo wa wafanyakazi wa kutekeleza shughuli fanisi za kampeni ya mawasiliano ya mabadiliko ya tabia na uhusiano. Mpango wa M&E pia uliruhusu shirika la Chifae kutambua mahitaji ya ziada ya uwezo wa kiufundi ya kuboresha ufanisi wa kampeni yake na ubora wa jumla wa mpango wake.

Hatua ya kutathmini kampeni ilisaidia pia shirika la Chifae kutambua mapengo muhimu yaliyokuwepo katika mbinu yake. Kwa mfano, shirika la Chifae linapanga kuzingatia zaidi masuala ya jinsia ili kuweza kujumuisha vizuri wanawake katika shughuli zake. Funzo hili lilijitokeza wakati utathmini wa kampeni ulitambua kuwa wanawake wachache zaidi walihojiwa kwa sababu ya vikwazo vya kitamaduni.