Ili kuhakikisha kuwa miradi ya P/CVE inabuniwa ili kuleta mabadiliko halisi, zingatia kubuni Nadharia ya Mabadiliko (ToC) ya kuelezea sababu na jinsi ambavyo mradi wako utatimiza malengo yako. Sehemu iliyo hapa chini inatoa maelezo ya msingi kuhusu shughuli na vidokezo muhimu vya kubuni ToC ambayo itakusaidia kupanga shughuli zako na kuzihusisha na mabadiliko unayolenga kuleta. Huenda tayari unatekeleza miradi ya kuzuia au kukabiliana na shughuli za VE. Katika hali hii, ToC inaweza kukusadia kuelezea kusudi la mradi wako na uhusiano wake na malengo ya mradi wa P/CVE. Ni fursa ya kubainisha iwapo unapaswa kurekebisha mbinu yako na kubuni upya mradi wako. Mchakato huu pia utasaidia katika kubuni mpango wa ufuatiliaji na utathmini (M&E), uliojadiliwa katika moduli ya Kufuatilia na Kutathmini.
Kulingana na shirika la USAID, Nadharia ya Mabadiliko (ToC) “inafafanua sababu na jinsi ambavyo mchakato wa mabadiliko unatarajiwa kutendeka na jinsi ambavyo shirika lako linanuia kujitahidi kuchangia moja kwa moja na/au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na kutimiza Kusudi la Mradi lililobainishwa.”
- Nadharia za mabadiliko ni kauli fupi ambazo zinafafanua mantiki na sababu ya msingi ya kusudi la mradi. Zinafafanua vipengele vya “nini, vipi na kwa nini” vya mabadiliko yanayotarajiwa.
ToC iliyobuniwa kwa umakini inapaswa kukusaidia:
- kufafanua mabadiliko na visababishi vinavyosababisha watu kushawishika kukubali dhana za itikadi kali na kujiunga na makundi hayo ndani ya mfumo wa eneo unaloshughulikia na sehemu za kuanzia kutekeleza shughuli mradi wako ndani ya mfumo huo;
- kubainisha kwa uwazi malengo ya mpango, yanayohusiana na uzuiaji na/au kukabiliana na shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu; na
- kuelezea kikamilifu sababu na jinsi ambavyo mradi utashughulikia mabadiliko na visababishi vya shughuli za makundi yenye itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu ili kutimiza malengo yake.
Mara nyingi nadharia za mabadiliko hubainishwa kama kauli za "ikiwa/basi"; "Tukifanya X (kitendo), basi tutasababisha Y (mabadiliko/mabadiliko ya kuleta amani, utulivu, usalama)." Ili kuhakikisha uzingatiaji wa mgogoro, inapendekezwa kuweka dhana na sababu ya msingi kuhusu ni kwa nini tunafikiria kwamba kitendo cha X kitasababisha matokeo ya Y, kwa kuweka Z – “kwa sababu.” Kauli hii ya “kwa sababu” inatumika kuangazia dhana zetu – na hatari husika–na jinsi ambavyo tutazishughulikia kupitia mpango.
VIDOKEZO VYA UTEKELEZAJI
Kabla ya kutunga Nadharia yako ya Mabadiliko, lifuatalo ni zoezi la kikundi la kukusaidia kuzingatia malengo ya mradi wako:
- Ni mwisho wa mradi na mwanahabari anaandika makala kuhusu mabadiliko makuu ambayo yameletwa na mpango wako. Ni mabadiliko gani ambayo mwanahabari ataandika kuyahusu? Ni sifa gani tatu ambazo zitaelezea mabadiliko haya?
- Andika mafanikio au malengo matatu makuu ambayo yamesababishwa na mpango. Weka majibu yanayofanana pamoja kulingana na mada husika. Kisha kagua na uyape kipaumbele malengo kama kikundi kikubwa. Kisha, weka pamoja dhana ambazo lazima ziwe za kweli ili kuweza kutimiza malengo haya yaliyopewa kipaumbele.
Nyenzo ya shirika la USAID ya Theories and Indicators of Change (THINC) Matrix inatoa muhtasari wa dhana kuu za mabadiliko katika shughuli ya udhibiti wa mgogoro, uzuiaji na usuluhishaji. Nyenzo ya THINC Matrix inaweza kukusaidia kubuni Nadharia yako ya Mabadiliko.